Marekani yaituhumu RSF kwa mauaji ya kimbari Sudan, yamuwekea vikwazo kamanda wake

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

XX

Marekani imegundua kuwa vikosi vya waasi wa RSF nchini Sudan na wanamgambo walioungana nao walitenda mauaji ya kimbari nchini Sudan, na kumwekea vikwazo kiongozi wa kundi hilo kufuatia mgogoro ambao umeua maelfu ya watu na kuwafanya mamilioni ya watu kukimbia makwao.

Vikwazo hivyo vinawalenga kumzuia kamanda wa RSF na familia yake kusafiri Marekani na kufungia mali zao.

Hatua hizi ni pigo kwa juhudi za RSF za kuboresha picha yake na kudai uhalali ikiwa ni pamoja na kuanzisha serikali ya kiraia wakati kundi hili la kijeshi likijaribu kupanua himaya yake zaidi ya nusu ya nchi wanayodhibiti sasa.

Hata hivyo, RSF inakanusha uhalifu dhidi ya raia na inadai kuwa wanaojihusisha na uhalifu ni watu wasiokuwa na udhibiti wa kundi hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema katika taarifa kuwa RSF na wandani wake wameendelea kushambulia raia, akiongeza kuwa walikuwa wakiua wanaume na wavulana kwa msingi wa kabila na kuwalenga wanawake na wasichana kutoka makabila fulani kwa ajili ya ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia.

Marekani awali iliwahi kuweka vikwazo dhidi ya viongozi wengine, pamoja na maafisa wa jeshi, lakini haikuwa imeweka vikwazo dhidi ya Dagalo, maarufu kama Hemedti, huku juhudi za kuleta pande zote mbili katika mazungumzo zikikwama kwa miezi ya hivi karibuni.

“Kwa kuwa ni kamanda mkuu wa RSF, Hemedti anawajibika kwa vitendo viovu na haramu vya vikosi vyake,” ilisema Idara ya Hazina ya Marekani.

Marekani pia ilipiga vikwazo vikampuni saba za RSF zilizoko UAE kwa kununua silaha. Hata hivyo, hatua hizi zinakuja kwa kuchelewa, kwani ni siku chache rais Joe Biden aondoke madarakani na huenda zitakuwa na athari kidogo kwa sera za Marekani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment