Jeshi la Uganda lakanusha wanajeshi wake kuuawa na wanamgambo wenye uhusiano na IS

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

c
Maelezo ya picha,Msemaji wa jeshi Meja Charles Kabona.

Jeshi la Uganda limekanusha madai kuwa wanajeshi wake 10 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la wanamgambo wa kundi la Islamic State Allied Democratic Forces (ADF), katika wilaya ya kati ya Kayunga.

Tovuti binafsi ya Chimp Reports iliripoti tarehe 6 Januari kuwa shambulio hilo lilitokea katika eneo la Misanga wilayani Kayunga, bila kutaja lini lilitokea.

“Hizi ni propaganda mbovu na zisizo na msingi zilizobuniwa na watu wabaya ili kutia hofu umma. Hakuna mauaji ya askari wetu huko Kayunga,” amesema msemaji wa jeshi Meja Charles Kabona.

“Eneo hilo ni la amani na wakazi wanaendelea na shughuli zao za kila siku katika mazingira tulivu.”

IS ilidai tarehe 5 Januari kupitia Telegram kwamba wanamgambo wake walipambana na wanajeshi wa Uganda huko Misanga tarehe 3 Januari wakati vikosi vya kijeshi “vilipojaribu kusonga mbele” kwenye maeneo ya kundi hilo katika eneo hilo.

ADF lililoundwa nchini Uganda lakini sasa lina makao yake makuu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaaminika kuwa limejiunga na kundi la IS.

Majeshi ya DR Congo na Uganda yamekuwa yakiendesha operesheni za pamoja dhidi ya ADF tangu 2021.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment