Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Chad imetamaushwa na kauli iliyotolewa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron dhidi ya viongozi wa Afrika.
Macron alisema kwamba viongozi wa mataifa ya Sahel ”hawana shukurani licha ya kusaidiwa kupambana na makundi ya kijihadi” huku wanajeshi wake wakindelea kuondoka za Afrika Magharibi.
Akimjibu Rais Macron, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Abderaman Koulamallah alisema “Afrika, ikiwemo Chad, iliisaidia Ufaransa kwa kiwango kikubwa wakati wa vita viwili vya dunia, jambo ambalo Ufaransa haijawahi kukubali,” tovuti ya habari ya Alwhida Info iliripoti.
Koulamallah alisema “viongozi wa Ufaransa wanastahili kuheshimu watu wa Afrika na kutambua thamani ya kujitolea kwao”.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko amepuuza jukumu la Ufaransa katika kuhakikisha nchi za Afrika zina uhuru, akiishutumu Paris kwa kufanya kinyume na hilo.
“Macron anajigamba kwamba “hakuna nchi ya Kiafrika ambayo leo ingekuwa huru kama haingesaidiwa na Ufaransa,” Sonko aliandika kwenye kwenye mtandao wake wa Facebook.
“Tutambue kwamba Ufaransa haina uwezo wala uhalali wa kuzihakikishia usalama na mataifa ya Afrika,” aliongeza, akiituhumu kwa kuchangia machafuko ya Libya na kuilaumu kwa kuchochea hali tete ya usalama katika Sahel.
Sonko alisema tangazo la Novemba 2024 kwamba Ufaransa itafunga kambi zake za kijeshi nchini Senegal lilitokana na ” juhudi za taifa hilo wa la Kiafrika kama nchi huru, inayojitawala”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.