Marekani yawapeleka wafungwa 11 wa Guantanamo Bay nchini Oman

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ghu

Wafungwa 11 kutoka Yemen katika jela ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo Bay yamepelekwa Oman.

Hatua hiyo imewaacha wafungwa 15 katika gereza hilo – ikiwa ni idadi ndogo zaidi katika wakati wowote katika historia ya jela hiyo.

Katika taarifa ya Idara ya Ulinzi iliishukuru Oman kwa kuunga mkono juhudi za Marekani “zinazolenga kupunguza idadi ya wafungwa na hatimaye kulifunga” gereza hilo.

Hakuna hata mmoja kati ya wanaume waliokamatwa baada ya shambulio la kigaidi la 9/11 aliyeshtakiwa kwa uhalifu wowote katika zaidi ya miongo miwili kizuizini.

Uhamisho huo, ambao inasemekana ulifanyika mapema siku ya Jumatatu, unakuja siku chache kabla ya mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, Khalid Sheikh Mohammed, atakapokiri makosa, kufuatia makubaliano na maafisa wa shirikisho ili kuepuka hukumu ya kifo.

Jela hiyo ya kijeshi ni sehemu ya kambi ya jeshi la wanamaji la Marekani kusini mashariki mwa Cuba. Ilianzishwa na utawala wa Bush mwaka 2002, kufuatia mashambulizi ya 9/11, ili kuwashikilia washukiwa waliokamatwa katika operesheni za kukabiliana na ugaidi. Katika kilele chake, ilishikilia wafungwa wapatao 800.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment