Umoja wa Mataifa: Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada Sudani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu zaidi ya Milioni 30 nchini Sudan, nusu wakiwa ni watoto wana uhitaji wa dharura wa misaada ya kibinadamu, baada ya maisha yao kutatizwa kutokana na vita vinavyoendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Mmoja wa wanamke wa Sudani waliotoroka makazi yao katika kambi ya Zamzam, Darfur Kaskazini, Sudan, Agosti 1, 2024.
Mmoja wa wanamke wa Sudani waliotoroka makazi yao katika kambi ya Zamzam, Darfur Kaskazini, Sudan, Agosti 1, 2024. REUTERS – Mohamed Jamal Jebrel

Umoja wa Mataifa, UN, unasema, ili kuwasaidia watu hao, Dola Bilioni 4.2 zinahitaji kutoka kwa wahisani, ili kuwafikia raia wa nchi hiyo zaidi ya Milioni 30.

Aidha, Umoja wa Mataifa unasema, kati ya watu hao, Milioni 20.9 wapo katika hali mbaya sana na wanahitaji msaada wa haraka kama chakula, maji safi, makaazi na dawa huku dunia ikionywa kuwa imeisahau Sudan na macho yote kuangazia Ukraine na vita vya Mashariki ya Kati.

Wito huu unakuja, baada ya hali ya ukame kutangazwa katika majimbo matano ya Sudan na hivyo kusababisha watu wengine zaidi ya Milioni 8 kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa kali.

Vita nchini Sudani vilivyoanza Aprili mwaka 2023 kati ya majenerali wawili wanaoataka kuongoza nchi hiyo, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, huku wengine zaidi ya Milioni 2.7 wakiyahama makaazi yao.

Watu wengine zaidi ya Milioni 3.3 wamevuka mpaka na kwenda kutafuta hifadhi katika mataifa jirani kama Chad na Sudani Kusini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment