Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza siku ya Jumatatu Januari 6, 2025 kwamba imewakabidhi Wayemeni kumi na mmoja wa Oman waliokuwa wanazuiliwa Guantanamo, gereza lenye utata lililoko kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Cuba, ambapo watu 15 sasa wanazuiliwa.

“Marekani inathamini nia ya Serikali ya Oman na washirika wengine kuunga mkono juhudi za sasa za Marekani za kupunguza kwa uwajibikaji idadi ya wafungwa na hatimaye kufunga kituo cha Guantanamo,” imesema taarifa ya Wizara ya Ulinzi.
Tangazo hili linakuja wiki moja baada ya mfungwa mwingine kuhamishwa kwenda Tunisia. Kati ya wafungwa 15 wanaosalia huko Guantanamo, watatu wanastahili kuhamishwa, watatu wanastahili kuchunguzwa ili kuachiliwa huru, saba wamefunguliwa mashtaka na wawili wametiwa hatiani, Wizara ya Ulinzi imesema.
Gereza la Guantanamo, lililofunguliwa mwaka wa 2001 na ambapo hadi wafungwa 800 walizuiliwa, kwa kiasi kikubwa limeharibu sifa ya kimataifa ya Marekani. Joe Biden, kama Barack Obama kabla yake, alikuwa ameelezea nia ya kufunga gereza hilo wakati wa mamlaka yake.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.