Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna MKWAMO ambao lazima uushughulikie leo kabla siku hazijaenda sana.
Mkwamo huu unatokana na HISIA zako kushikiliwa mahali ambapo sio sahihi tena.
Na mara nyingi ni kwa sababu HAUJAKUBALIANA na matokeo.
Ni kweli kwa mawazo yako ulikuwa unadhani utakaa katika hiyo ofisi kwa muda mrefu, ila kuna jambo limetokea imebidi uondoke.
Usiendelee kushikilia huo uchungu.
Anza Upya Na Songa Mbele.
Inawezekana ulijua utapanda hadi ngazi ya juu katika hiyo taasisi au chama.
Na kwa sababu hii, ulijitolea sana kila ulichonacho na kufanya kwa bidii, ila hakuna mtu amekumbuka yote hayo na leo imebidi uondoke.
ACHILIA!
.
Pengine ni mtu ambaye ulijua utazeeka naye.
Ulijitolea kila ulichonacho tena kwa kujinyima.
Matokeo yake mambo yameenda ndivyo sivyo na inabidi muachane.
Usiendelee kung’ang’ania usipohitajika ama ambapo lazima uondoke.
Fungua ukurasa mpya!
.
Kuna watu wengi sana kinachowakwamisha ni kwa sababu, baada ya kitu fulani kutokea wameshindwa kabisa kuendelea mbele.
Wanavutwa na hisia za zamani na wanakataa uhalisia kwamba inabidi waanze upya.
Leo, Amua kwa makusudi Kusahau yaliyopita na Uanze Upya.
Kuna makubwa yako mbele yako yanakusubiria uachilie yaliyopita ili MILANGO MIPYA IFUNGUKE.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.