Kama ulizaliwa ukoo wa laana baada ya Kumpokea Yesu laana inaishia hapo.

Kama ulizaliwa ukoo wa laana baada ya Kumpokea Yesu laana inaishia hapo.
Kama ulizaliwa ukoo maskini umaskini unaishia pale ulipo mpokea Yesu.
Kama ulizaliwa ukoo ambao hakuna anayeweza pata mtoto au kukaa na familia kuanzia umempokea Yesu amini wewe sio kama wao
Kabla Yesu kuja Duniani tulikua katika laana ya Dhambi lakini Mungu alitupenda zaidi akamleta mwanae Yesu duniani kwaajiri ya ukombozi ile damu iliyomwagika msalabani ndio ulikua ukombozi wako na ndio maana neno linasema kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Damu ya asili ndiyo inayotesa watu wengi kila ukoo kuna asili yao,hiyo ni damu inakua inawafatilia ndio maana Yesu akaja duniani amwage damu yake ili kuvunja maagano na kufuta damu zile za ukoo.
Ninakuombea leo Damu ya Yesu ibadili maisha yako na utafanikiwa hata kama kwenu hawajawahi kufanikiwa.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment