Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Korea Kaskazini imerusha kombora linaloonekana kuwa la masafa ya kati kuelekea bahari ya mashariki, jeshi la Korea Kusini lilisema, ikiwa ni hatua ya kwanza ya Pyongyang katika kipindi cha miezi miwili.
Kombora hilo lilipaa kilomita 1,100 kabla ya kuanguka baharini, jeshi lilisema, na kuongeza kuwa “linalaani vikali” “kitendo hiki cha wazi cha uchochezi”.
Hatua hiyo inakuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiitembelea Seoul kwa mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu wa Korea Kusini.
Mapema Jumatatu, Blinken alikutana na kaimu rais Choi Sang-mok, ambapo alielezea muungano kati ya Washington na Seoul kama “msingi wa amani na utulivu kwenye rasi ya Korea”.
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa limeimarisha ufuatiliaji kwa ajili ya kudhibiti hatua za Korea Kaskazini siku zijazo na “linashiriki kwa karibu habari” ya kurushwa kwa kombora la leo na Marekani na Japan.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.