Mungu anataka kukutumia,na yuko tayari kukujibu kwa kila uliombalo kwakua ni ahadi yake amesema ombeni nanyi mtapewa,kwanini haupokei kuna sababu.Kuna vitu vinavyo kufanya usipokee Gidioni alikua anatoka katika ukoo masikini sana na alikua ana mjua Mungu lakini Mungu pia alitaka kumtumia alimwambia ili ule ushujaa uliondani yako watu wauone lazima uvunje madhabahu za miungu zilizopo kwenu,kabla hajamtumia Ibrahamu Mungu alimwambia ondoka uvuke ng’ambo ya pili hakutaka tena Ibrahim aendelee kuabudu miungu.Hata wewe ni kweli unasali na unampenda na kumwabudu Mungu lakini kuna katabia Mungu anataka uziache kwanza hapo utamuona Mungu anatenda haraka,unamuomba Mungu lkn kwako kuna madawa ya kienyeji unayatumia,unakuomba Mungu lakini biashara zako umezindika kwa nguvu za giza,ni kwel una muabudu Mungu na kila siku upo kanisani lkn ni muongo sana,unamuamini Mungu lakini unapenda kunung’unika sana.Amini nakwambia ukiacha tabia ambayo hazimpendezi Mungu utamuona Mungu akijibu na kutenda kwa wakati wala hatakawia kusikia sala zako.
Hawakuwekwa watu special kwaajiri ya kuhubiri Injiri bali ni kila mmoja aliye mwamini kristo.
Maneno ya mwisho ya Yesu duniani wakati anapaa kwenda mbinguni akasema Enendeni Duniani kote mkaihubiri injiri.
Kuna watu hawawezi hata kukemea ubaya kwa mtu wakizani hiyo sio kazi yao.Wote waliomuamini Mungu huwekewa roho ya msukumo wa kutamka jambo kwa aliye na uhitaji.Usipende kula peke ako unapolishwa wape na wengine usiwe mchoyo.Mungu anataka ufanane nae. Wafundishe watu habar za ufalme wa Mungu waambie kuhusu Mungu wako unaye muabudu,waeleze jinsi alivyokuponya na kukupa faraja kwenye maisha yako.
Hizi habari za uzima na baraka alitakiwa aje aseme Mungu mwenyewe lkn kwasababu yy ni mfalme Mungu wa miungu yote anawapa kazi watu wake ili wamnadi na watu wake ni ww na mimi,ukimuokoa mtu kwa neno la uzima utabarikiwa sana
Mambo mengine Mungu huyatoa kwenye maisha yako kwakutamka neno la baraka na uzima kwa mtu mwingine,utashangaa yale matatizo yaliyokuwa yanakusumbua yametoweka yote kwakufanya hivyo unaujenga mwili wa Kristo na hautabaki kama ulivyo.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.