Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Kenya, hali ya kutokuwa na uhakika inatawala katika mkesha wa kuanza kwa mwaka wa masomo. Mwanzoni mwa mwezi Desemba, baada ya kutokea moto mkubwa katika shule ya bweni katikati mwa nchi, Wizara ya Elimu ilitangaza kufungwa kwa shule karibu 350 za bweni, kutokana na kushindwa kwao kufikia viwango vya usalama.

Shule zilizofungwa zilikuwa na mwezi mmoja kurejea kwenye kiwango cha usalama. Lakini katika mkesha wa kuanza kwa mwaka wa masomo, hakuna mtu nchini Kenya anayejua ni shule ngapi za bweni zitaweza kufungua tena milango yao.
Wakati huo huo, kwa serikali ya Kenya, hakuna maelewano yanayowezekana. Shule za bweni ambazo hazifikii viwango vya usalama zitasalia kufungwa hadi ilani nyingine. Haya yalibainishwa wiki hii na mkurugenzi katika Wizara ya Elimu, Julius Ogamba, kabla ya kuongeza kuwa juhudi zote zinafanywa kuhakikisha wanafunzi na waalimu wanaurudi shuleni katika mazingira bora. Wizara ya Elimu, hata hivyo, haikuweza kutoa takwimu sahihi kwa idadi ya shule za bweni ambazo zinaendelea kufungwa.
Jumuiya ya Kitaifa ya Wazazi inaunga mkono uamuzi huu wa serikali. “Hatuwezi kucheza na maisha ya watoto wetu,” aanasema kiongozi wake, Silas David Obuhadsa.
Hata hivyo, kutokuwa wazi kwa hali hiyo kunatia wasiwasi. Suala la ada za uhamisho kwa wanafunzi ambao hawataweza kurejea katika shule zao za awali, hasa, huzua wasiwasi, kwa sababu “wazazi tayari wanatatizika kupata riziki,” anaongeza Silas David Obuhadsa. Wiki tatu zilizopita, Muungano wa Shule za Kibinafsi nchini Kenya uliahidi kuwa shule zilizofungwa zitaboreshwa katika kiwango cha mwanzo wa mwaka wa masomo. Lilipowasiliana na RFI, shirika hilo halikutaka kujibu maswali yetu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.