Sudani: Hali ya kibinadamu yazidi kuzorota baada ya zaidi ya miezi 20 ya vita.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wito wa kusitisha mapigano nchini Sudan unaongezeka ikiwa ni mwanzo tu wa mwaka 2025. Wakuu wa Nchi, Umoja wa Mataifa, Masirika yasiyo ya kiserikali: wote wanawataka pande mbili hasimu katika mgogoro wa Sudani, mkuu wa jeshi la serikali Jenerali al-Burhan, na kiongozi wa wanamgambo Jenerali Hamdane Dogolo anayejulikana kama Hemedti, kuweka chini silaha zao na kuweka mbele mazungumzo. 

Raia wa Sudan waliokimbia ghasia zinazozidi kuongezeka katika jimbo la al-Jazirah wamepumzika kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa mashariki wa Gedaref, Novemba 23, 2024.
Raia wa Sudan waliokimbia ghasia zinazozidi kuongezeka katika jimbo la al-Jazirah wamepumzika kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa mashariki wa Gedaref, Novemba 23, 2024. AFP – –

Hata hivyo, nchi hiyo inaingia katika mwezi wake wa 21 wa vita na, kulingana na Umoja wa Mataifa, ni mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

Zaidi ya miezi 20 ya vita na pande mbili hasimu ambazo kila moj ainashikilia msimamo wake nchini Sudani: kupata uongozi wa kijeshi. Katika hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya uhuru wa Sudani, Januari 1, 2025, Jenerali al-Burhan, mkuu wa jeshi na rais wa Baraza Kuu, kwa mara nyingine tena alifutilia mbali ushirikiano wowote na mpinzani wake, Jenerali Hemedti, mkuu wa wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). “Hatuwezi kukubali kuwepo kwa wauaji na wahalifu hawa [FSR] na wasaidizi wao, miongoni mwetu,” amebainisha tena wakati wa hotuba yake kwa njia ya televisheni.

Cchi imegawanyika katika sehemu mbili, huku RSF ikidhibiti magharibi mwa nchi nzima, majimbo tofauti ya Darfur, na majimbo ya kusini. Jeshi linadhibiti mashariki mwa nchi, majimbo ya White Nile na Blue Nile, Sennar, Gedaref, Kassala.

Leo, sehemu kubwa ya mapigano imejikita katika maeneo matatu. Kuna mji mkuu, Khartoum, ambao bado umegawanyika mara mbili lakini ambapo jeshi limepata nguvu katika miezi ya hivi karibuni, haswa huko Omdurman, mji pacha wa Khartoum, na pia katika wilaya kubwa ya Bahri kaskazini mwa katikati mwa mji. Mapigano pia yanatokea kusini mwa Khartoum, katika majimbo ya Sennar na al-Jazirah, ambayo ni vikapu vya chakula nchini humo na ambapo RSF inashutumiwa kuharibu makumi ya vijiji katika miezi ya hivi karibuni. Na, hatimaye, huko el-Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, kwenye mpaka na Chad. Mji mkuu wa mwisho huko Darfur ambao bado uko mikononi mwa jeshi, el-Fasher umezingirwa na wanamgambo kwa miezi 8 na labda unakumbwa na mapigano makali zaidi ya vita hivi. Ni katika eneo hili ambapo Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi kuanza kwa njaa miezi michache iliyopita.

Ukosefu mkubwa wa chakula

Umoja wa Mataifa umeitaja Sudani kuwa katika mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. Mwishoni mwa mwezi wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumiwa Wakimbizi (UNHCR) lilirekodi zaidi ya Wasudani milioni 8.7 waliokimbia makazi yao nchini humo. Kwa takwimu hii wanaongezwa wakimbizi milioni 3.2 ambao wameondoka nchini na wako katika nchi jirani: milioni 1.2 nchini Misri, 900,000 nchini Sudani Kusini, 720,000 nchini Chad; pamoja na LibyaUgandaEthiopia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Najaa ambayo ilitangazwa rasmi miezi michache iliyopita katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam huko Darfur Kaskazini, imeenea katika mikoa mitano ya ziada: kambi tatu za wakimbizi huko Darfur Kaskazini, eneo la Milima ya Nuba, na kusini mwa nchi. Na inatishia zaidi ya watu 630,000, kulingana na ripoti kutoka IPC, mfumo wa uainishaji wa usalama wa chakula unaotumiwa na Umoja wa Mataifa.

Misaada ya kibinadamu ambayo haifiki

Mnamo Aprili 15, 2024, mwaka mmoja tu baada ya kuanza kwa vita, Ufaransa ilipanga mkutano wa nchi wafadhili huko Paris ambao ulifanya iwezekane kukusanya euro bilioni 2 kwa Sudani. Ufadhili huo hautoshi, wengine wanaeleza: tuko mbali na bilioni 3.8 zilizoombwa na Umoja wa Mataifa.

Na ili kutoa misaada, kunahitajika usitishaji mapigano, mipaka iwe wazi, na uwezo wa kutoa msaada huu, wahusika wa masuala ya kibinadamu wanabainisha. Ili kufikia kambi ya wakimbizi ya Zamzam huko Darfur Kaskazini, lori za misaada lazima, kwa mfano, ziondoke Adré kwenye mpaka wa Chad, zikivuka maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment