Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mapigano makali kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na Wanajeshi wa Kongo, wanaoungwa mkono na makundi yenye silaha, yametokea siku ya Alhamisi, Januari 2, mashariki mwa DRC. Mapigano hayo makali yametokea katika miji kadhaa katika eneo la Masisi, takriban kilomita 70 magharibi mwa mji wa Goma, na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao siku moja baada ya sherehe za Mwaka Mpya.

Siku nzima ya Alhamisi, Januari 2, milio ya silaha nyepesi na nzito ilisikika hata katika miji ya Kaniro na Kinigi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.
Kulingana na mashirika ya kiraia ya Kongo, mapigano haya makali yalifanyika karibu kabisa na Katale, eneo lililoko takriban kilomita ishirini kusini mashariki mwa Masisi, kituo kikuu cha utawala cha eneo hilo ambacho kingetamaniwa na waasi wa M23, kulingana na vyanzo kadhaa vya habari. Katale, ambako kuna ngome ya kimkakati ya jeshi la Kongo na washirika wake, Wazalendo, ni kizuizi cha mwisho katika barabara ya Masisi.
Mapigano yasababisha mamia ya wakaazi kukimbia vijiji vyao
Wakati mapigano kati ya jeshi na waasi pia yanaripotiwa katika maeneo kadhaa ya kichifu cha Bashali, Alphonse Mushesha Mihingano, mkuu wa eneo jirani la Buabo, anasema kuwa mapigano haya yamesababisha mamia ya wakazi kukimbia vijiji vyao. Msemaji wa wazalendo waliopo katika eneo hilo, Kanali Séraphin Nsabimana, kwa upande wake, anawashutumu wapiganaji wa M23 kwa kushambulia maeneo yao.
Mapigano makali yameanza tena huko Kivu Kaskazini tangu kushindwa kufanyika kwa mkutano wa kilele mjini Luanda ambao ulipaswa kuwaleta pamoja rais wa Kongo, Felix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, Desemba 15, nchini Angola.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.