Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Jeshi la Israeli limehapisha,siku ya Alhamisi, Januari 2, data juu ya hasara iliyopatikana kwa miaka ya 2023 na 2024. Jeshi la Israeli limetangaza kuwa wanajeshi 921 wa Israel walipoteza maisha katika kipindi hiki. Wakati wanajeshi wasiopungua 891 wameuawa tangu mashambulizi ya Oktoba 7, 2023, idadi ya watu waliojiua pia imefikia rekodi tangu miaka 13 iliyopita.

Shambulio la kushtukiza la Hamas dhidi ya vijiji vinavyozunguka Ukanda wa Gaza, na vile vile kwenye vituo vya kijeshi, lilisababisha vifo vingi ndani ya jeshi la Israeli: Wanajeshi 329 waliuawa wakati wa matukio mabaya yaliyotokea siku hiyo. Kisha, baada ya kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israeli katika Ukanda wa Gaza, wanajeshi 390 walikufa wakati wa mapigano katika eneo la Palestina.
Mzozo na Lebanon pia ulisababisha hasara kwa upande wa jeshi la Israeli. Katika pande zote mbili za mpaka, wanajeshi 37 waliuawa kwenye eneo la kaskazini, ikiwa ni kutokana na mapigano na Hezbollah, lakini pia kutokana na mashambulizi ya roketi na ndege zisizo na rubani. Jeshi bado linasema kuwa wanajeshi 11 walifariki katika Ukingo wa Magharibi wakati huo huo, idadi kubwa zaidi ya hasara kwenye uwanja wa vita ndani ya nchi nje ya maeneo halisi ya mapigano.
Lakini ripoti hii pia inabainisha ongezeko la kesi za kujiua kwa askari: angalau 38 kati yao walijiua mnamo mwaka 2023 na 2024, idadi ya rekodi kwa miaka 13. Sababu za watu hao kujiua hazikubainishwa; Ripoti inasema tu kwamba sio lazima kuhusiana na vita. Jeshi linahusisha idadi hii kubwa kwa sehemu na uhamasishaji mkubwa wa askari wa akiba.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.