Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Afisa wa Polisi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo anatuhumiwa kuwaua raia wawili wa China na kumjeruhi mwingine katika jimbo la Lomami kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeripoti tovuti ya Radio Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.
Polisi huyo alikuwa na jukumu la kuwalinda wafanyakazi wa China wa kampuni ya Crec 6, inayoendesha ujenzi wa miundombinu ya barabara.
“Polisi mmoja aliwapiga risasi wafanyakazi watatu wa Kichina wa Crec 6 siku ya Jumatano, tarehe 1 Januari huko Mwene-Ditu, jimbo la Lomami. Aliwaua wahamiaji hao wawili papo hapo na kumjeruhi vibaya mwingine,” amesema Kanali Justin Bora Uzima, mwendesha mashtaka wa kijeshi katika eneo hilo.
Redio Okapi imeripoti kuwa sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana, lakini walioshuhudia walizungumza kuhusu mzozo wa nyama ya ng’ombe wakati wa sherehe za mwisho wa mwaka.
Afisa wa polisi anayeshukiwa amekimbia.
Meya wa mji wa Mwene-Ditu, Gérard Tshibanda Kabwe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa baadaye.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.