Shamsud-Din Jabbar: Je, aliyetekeleza mashambulizi ya New orleans ni nani?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

f

FBI imemtaja mshambuliaji kuwa Shamsud-Din Jabbar mwenye umri wa miaka 42 – mwanajeshi mkongwe na raia wa Marekani kutoka Texas.

Kulingana na wasifu wake wa LinkedIn ambao sasa umeondolewa, Jabbar alikuwa amefanya kazi katika majukumu mbalimbali katika Jeshi la Marekani, ikiwa ni pamoja na katika kitengo cha rasilimali watu na teknolojia ya mawasiliano (IT).

Alipelekwa Afghanistan kuanzia Februari 2009 hadi Januari 2010.

Katika video ya YouTube iliyotumwa mwaka wa 2020, Jabbar alisema kuwa wakati wake jeshini ulimfundisha “maana ya utumishi bora na maana ya kuwa msikivu na kuchukulia kila kitu kwa uzito, ili kuhakikisha kuwa mambo yanafanyika bila kasoro”, CBS inaripoti.

Alisoma katika Chuo Kikuu cha George State kuanzia mwaka 2015 hadi 2017, na kuhitimu shahada katika Mifumo ya mawasiliano ya Kompyuta.

CBS inaripoti kuwa alioa mara mbili. Ndoa yake ya kwanza iliisha mnamo 2012 na ya pili ilidumu kuanzia mwaka 2017 hadi 2022.

Anaonekana pia kufanya kazi katika mali isiyohamishika, akiwa na leseni ambayo muda wake uliisha mnamo 2021.

Jabbar alikuwa na rekodi ya uhalifu, inayohusiana na makosa ya barabarani na wizi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment