Korea Kusini: Rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol apinga kukamatwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Korea Kusini, agizo la kukamatwa kwa rais linaweza kutekelezwa leo Alhamisi, Januari 2, kulingana na shirika la habari la Yonhap. Mkuu wa nchi amesimamishwa kazi, lakini bado anashikilia rasmi wadhifa wake. Yeye ndiye rais wa kwanza aliye madarakani katika historia ya Korea Kusini kuwa chini ya hati ya kukamatwa. Hii inaweza kutekelezwa wakati wowote.

Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol wakiandamana mbele ya makazi ya rais mjini Seoul, Desemba 31, 2024.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Yoon Suk-yeol wakiandamana mbele ya makazi ya rais mjini Seoul, Desemba 31, 2024. AP – Lee Jin-man

Yoon Suk-yeol anatuhumiwa kwa “uasi” na “matumizi mabaya ya mamlaka” kwa kujaribu kuanzisha sheria ya kijeshi katika nchini Korea Kusini mnamo Desemba 3. Alitakiwa kuhojiwa, lakini hakutokea alipoitwa na wachunguzi. Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani alipinga Alhamisi kwa siku ya tatu kufuatia kukamatwa kwake, na kuapa “kupambana hadi mwisho” dhidi ya mamlaka zinazotaka kumhoji kuhusu jaribio lake lililoshindwa la kuweka sheria ya kijeshi.

Ofisi Kuu ya Upelelezi wa Ufisadi (CIO), ambayo inafanya uchunguzi wa mapinduzi ya Desemba 3, ina hadi Januari 6 kutekeleza hati ya kukamatwa iliyotolewa na mahakama ya Seoul dhidi ya Yoon Suk -yeol. CIO imeomba kibali cha kukamatwa baada ya rais aliyeng’olewa mamlakani kupuuza wito tatu mfululizo za kuhojiwa. Idara ya usalama ya rais, ikitaja siri za ulinzi, hata hivyo inazuia wachunguzi kuingia nyumbani na katika ofisi ya Yoon Suk-yeol kufanya msako.

Mvutano unaongezeka

Mbele ya makazi ya rais, katika wilaya ya Hannam ya Seoul, mvutano unaongezeka. Idadi kubwa ya polisi inapiga kambi katika eneo hilo: karibu mabasi kumi na tano, vizuizi vya barabarani, maafisa kadhaa, anaripoti mwandishi wetu huko Seoul, Camille Ruiz. Tangu agizo la kukamatwa lilipotolewa siku ya Jumanne, wafuasi na wapinzani wa Yoon Suk-yeol wamekuwa wakiandamana karibu kila mara karibu na makazi yake huko Seoul, wakirushiana matusi huku maafisa wa polisi wakikaa katikati ya pande hizo mbili.

Vyombo vya habari vya ndani, ikiwa ni pamoja na vituo kadhaa vya televisheni, vinafanya kazi kwa bidii ili kunasa picha za kihistoria za uwezekano wa kukamatwa kwa rais. Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi wa Maafisa Waandamizi inaweza kujaribu kutekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa dhidi ya rais aliyeondolewa madarakani leo Alhamisi.

Lakini kufanya hivyo kunaweza kukabiliana na vikwazo kadhaa. Kwanza, wafuasi wa rais, ambao wanaandamana mbele ya makazi. Usiku wa Januari 1 kamkia 2, Yoon Suk-yeol amewatumia barua ya kuwashukuru. Kikwazo cha pili ni ulinzi wa rais, ambao tayari umezuia uchunguzi mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni.

Hati ya kukamatwa inaisha Januari 6. Ikiwa Yoon atakamatwa, wachunguzi wana saa 48 kupata hati ya pili ya kukamatwa au kumwachilia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment