Marekani: Kumi na tano waangamia katika shambulio New Orleans, mtuhumiwa wa uhalifu atambuliwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Takriban watu 15 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati gari lilipoingia kwenye umati wa watu na kugonga watui kadhaa katika eneo la watalii la New Orleans, nchini Marekani, mamlaka ya jiji la Marekani imetangaza Jumatano Januari 1. Mtuhumiwa wa shambulio hilo mbaya ametambuliwa.

Maafisa wa idara ya Huduma za dharura wakiwa kaika Mtaa wa Bourbon Street baada ya gari kugonga umati wa watu kwenye Mtaa wa Canal na Bourbon huko New Orleans, Jumatano, Januari 1, 2025.
Maafisa wa idara ya Huduma za dharura wakiwa kaika Mtaa wa Bourbon Street baada ya gari kugonga umati wa watu kwenye Mtaa wa Canal na Bourbon huko New Orleans, Jumatano, Januari 1, 2025. AP – Gerald Herbert

Dereva alitaka kugonga”watu wengi” iwezekanavyo wakati wa shambulio hili la gari, kulingana na polisi. Maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa kwa risasi. Mtuhumiwa wa uhalifu amefariki, vituo viwili vya televisheni vya Marekani vimeripoti, vikinukuu vyanzo vya polisi.

Shambulio hilo lilitokea usiku wa manane, saa 9:15 asubuhi, katika eneo lenye watu wengi ambapo watu walikuwa wakisherehekea Mwaka Mpya, kati ya Mtaa wa Canal na Bourbon, katika wilaya ya kihistoria na ya sherehe, inayojulikana kama “French Quarter” (“mtaa wa Ufaransa”). Wilaya hii inajulikana kwa mikahawa yake, baa na vilabu vya muziki wa jazz, pia ni eneo linalotembelewa na watu kutoka jamii ya wapenzi wa jini moja (LGBT).

Jiji hili la New Orleans na French Quarter inawakilisha mahali ambapokunaripotiwa mchanganyiko wa tamaduni , ambapo kuna pombe, ambapo pia kuna uhuru fulani wa kufanya mapenzi […] na kwa ujumla hii haifurahishi watu wote, wenye msimamo wakidini , Mkristo au Muislamu.

Kulingana na mashahidi walionukuliwa na CBS News, lori liliingia kwenye umati kwa “mwendo mkali” kabla ya dereva wake kuruka kutoka kwenye gari na kufyatua risasi kwenye umati, na kusababisha polisi kujibu.

Mtuhumiwa atambuliwa

FBI imethibitisha utambulisho wa mtuhumiwa wa shambulio hilo: Shamsud-Din Jabbar, mwanajeshi wa zamani wa Marekani mwenye umri wa miaka 42. Bendera ya kundi la Islamic State ilipatikana kwenye gari hilo, FBI imeandika katika taarifa yake. “Silaha na kifaa kinachowezekana cha IED [kifaa cha kulipuka] vilipatikana kwenye gari la mshambuliaji,” inaongeza Ofisi ya Shirikisho ya Uchunguzi.

FBI pia imebaini kwamba mshukiwa huyo alikuwa mwanajeshi wa zamani. “Ni mwanajeshi mustaafu, tunaamini aliondoka jeshi akiwa katika hali nzuri, lakini tunajitahidi kupata taarifa zote hizo,” afisaa wa FBI Alethea Duncan amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari. “Hatuamini kwamba Shamsud-Din Jabbar aliwajibika peke yake,” ameongeza.

Vyombo vya habari kadhaa vya Marekani, ikiwa ni pamoja na Associated Press na Fox News, vilifichua saa kadhaa mapema utambulisho wa dereva wa gari hilo na vimeonyesha kuwa wachunguzi walikuwa wanafanya kazi ya kukusanya taarifa za ziada kuhusu historia ya Shamsud-Din Jabbar na kwenye bendera nyeusi iliyokuwa ndani ya gari.

“Shambulio la kigaidi”

LaToya Cantrell, meya wa jiji hilo, ametangaza kuwa ni “shambulio la kigaidi.” Rais wa Marekani Joe Biden kisha amesema kwamba “saa chache kabla ya shambulio hilo”, mshukiwa “alirusha video kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha kwamba alihamasishwa na Islamic State”. Video hizi pia zinashuhudia “nia ya kuua”, ameongeza, katika hotuba kutoka kwa makazi ya Camp David, karibu na Washington.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment