Mungu ana mipango mizuri na maisha yako.

Mungu anajua nini unastahili kupata,kama Baba alikwisha kuandaa misingi ya maisha yako ili yawe bora.Kuna muda unaweza kuomba lakini ukaona hupokei majibu,
unaweza ukawa unaomba Mke au Mume kumbe unaye omba awe mume wako Mungu amesha muona ni nyoka atakugonga,au unatamani kazi fulani ukiingia kwa maombi una msihi Mungu akupe hiyo kazi kumbe Mungu amekwisha ona kupitia hiyo kazi maisha yako yataharibika utakutana na marafiki watakao haribu maisha yako.Kuna jambo baya ulipata baada ya kulazimisha kufanya jambo ambalo sio mpango wa Mungu au baada ya kuona hujibiwi ukapita njia nyingine kutafuta majibu ndipo ulipata shida kwenye maisha hako.

Yeye ni Baba ambaye ukimuomba samaki hawezi kukupa nyoka wala hawezi kukupa Jiwe badala ya mkate,jifunze kuomba katika Roho ndipo utakapo uona ushindi wako na kila utakacho omba katika Roho utapata kwakua ndiyo mapenzi ya Mungu.
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
#CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment