Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Guinea, “2025 utakuwa mwaka wa uchaguzi” ametangaza Rais Mamadi Doumbouya kwenye televisheni ya taifa wakati wa kuukaribiha Mwaka Mpya. Kwenye ajenda: uchaguzi wa wabunge, wa urais na wa serikali za mitaa pamoja na kura ya maoni ya kupitishwa kwa Katiba mpya.
Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba na baada ya kampeni ya sensa na tathmini ya vyama vya siasa nchini, serikali imebainisha kufutwa kwa vyama au kusimamishwa kwa 50% ya vyama hivyo. Siku ya Jumanne, Desemba 31, Rais wa Guinea Mamadi Doumbouya ametangaza kurejesha jumla ya shughuli za kisiasa kwa kuzingatia chaguzi hizo.
Katika hotuba yake, Jenerali Doumboya amebanisha dhamira yake ya kuimarisha misingi ya amani, muhimu kwa ustawi wa taifa: “Ninathibitisha dhamira yangu ya kuendelea kuimarisha misingi ya amani hii muhimu kwa ustawi wa taifa letu. Ninawaalika raia wa Guinea, ambao hisia zao za juu za uzalendo na uwajibikaji ni wa kupigiwa mfano, kukuza zaidi udugu, mshikamano na uvumilivu. “
Pia ametoa wito kwa wadau wa kisiasa, akiwataka kutanguliza masilahi ya juu ya Guinea katika vita vyao vya kisiasa: “Ninawaomba kaka na dada zangu, wadau wa kisiasa, waiangalie kwanza Guinea, kuhifadhi masilahi ya juu ya raia wa Guinea katika mapambano yao ya kisiasa. Kwa pamoja, tuhakikishe kwamba mashauriano mbalimbali ya uchaguzi yanafanyika katika hali bora kabisa, kwa amani na utulivu kamili ili kuonyesha ulimwengu sura ya Guinea iliyoungana iliyodhamiria kujenga mustakabali wake katika utulivu na demokrasia. “
Katika miaka ya hivi karibuni, watu kadhaa walipoteza maisha yao nchini. Rais amekumbusha kwamba majanga haya yalihusishwa na maandamano ya kisiasa ya hapo awali na umuhimu wa kudumisha utulivu wa umma: “Nchi yetu imekumbwa na majanga yanayohusiana na maandamano ya kisiasa kwa muda mrefu. Mamlaka ya serikali mara kwa mara ilipuuzwa, utulivu wa umma ulivurugwa na usafirishaji huru wa bidhaa na watu kuathiriwa. Hali hii ilisababisha CNRD kuchukua majukumu yake na kupunguza kwa muda shughuli za kisiasa nchini nzima. “
Mwaka 2025 ukiwa ni mwaka wa uchaguzi, ametangaza kurejesha jumla ya shughuli za kisiasa ambazo hadi sasa zimejikita katika makao makuu ya vyama vya siasa: “Baada ya muda wa uchunguzi na baada ya kushauriana na wananchi wenzetu, jumla ya shughuli za kisiasa zitarejea kuanzia mwaka wa 2025.” Lakini urejeshaji huu unatokana na heshima kwa mamlaka ya Serikali: “Urejesho huu lazima ufanyike kwa heshima ya taifa, taasi za uongozi wa nchi, vikosi vya usalama na utulivu wa umma na kufuata sheria zinazosimamia utekelezaji wa shughuli za kisiasa. “
Rais Doumboya ameonya kwamba hatasita kuingilia kati tukio la uvunjifu wa amani wa umma au tishio kwa umoja wa kitaifa: “Serikali, kwa hali zote, haitasita kuchukua majukumu yake iwapo utulivu wa umma utavurugwa, vitisho au uvunjifu wa amani, vitisho au kushambulia umoja wa kitaifa. “
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.