Kipenga Cha Michezo-Mwaka 2024 : Habari Kuu za Michezo Zilizotikisa Dunia Viwanjani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Olimpiki za Paris iliangaza majira ya joto kwa matukio ya kusisimua. Rekodi zilivunjwa, na mashujaa walijitokeza katika michezo tofauti kuanzia kwenye soka, riadha, ngumi, voliboli, basketiboli na michezo mingine mingi.

El ecuatoriano Brian Daniel Pintado, celebra después de ganar la medalla de oro al final de la marcha masculina de 20 km en los Juegos Olímpicos de Verano de 2024, el jueves 11 de agosto de 2019. 1 de enero de 2024, en París, Francia.
El ecuatoriano Brian Daniel Pintado, celebra después de ganar la medalla de oro al final de la marcha masculina de 20 km en los Juegos Olímpicos de Verano de 2024, el jueves 11 de agosto de 2019. 1 de enero de 2024, en París, Francia. AP – Vadim Ghirda

Tunapofunga mwaka 2024, ni wakati wa kutafakari matukio makubwa ya michezo yaliyoteka hisia za ulimwengu na walimwengu. Kwa kweli siku zinaenda mbio jana ilikua januari Mosi leo mwaka 2024 ni kwaheri. Kutoka AFCON hadi EURO, Olimpiki, Ndondi za uzito wa juu, Ligi ya Mabingwa CAF, na tenisi, hapa kuna habari kuu za mwaka huu:

AFCON 2024 : Mashindano ya Soka Barani Afrika

Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) lilirejea kwa burudani ya hali ya juu, likionyesha vipaji bora zaidi barani. Mwenyeji Ivory Coast walitawala, huku vigogo kama Ghana wakipata mshtuko wa kuondolewa mapema mataifa kama Cape verde yakitoa burudani ya kipekee.

CAF (Shirikisho la Soka Barani Afrika) liliripoti faida ya dola milioni 72 kutoka Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024. Hii inaonyesha mafanikio makubwa ya kibiashara kwa soka la Afrika katika ngazi ya kimataifa.

Taji la Kombe la Mataifa ya Afrika
Taji la Kombe la Mataifa ya Afrika © CAF

Kwa mwaka wa fedha wa 2024-2025, CAF inatarajia mapato ya karibu dola milioni 150, huku matumizi yakikadiriwa kuwa dola milioni 138.2, na hivyo kutabiri faida halisi ya dola milioni 11.7 – faida ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

UEFA EURO 2024: Tamasha la Soka Ulaya

Mashindano ya UEFA EURO 2024 yalifanyika nchini Ujerumani, yakileta pamoja mataifa bora ya soka barani Ulaya. Timu ya taifa la Hispania wakawa washindi kwa kuishinda England katika fainali ushindi wa kihistoria kwa timu ambayo ilijaa wachezaji damu changa.

Rodri avec le trophée de l'Euro 2024.
Rodri avec le trophée de l’Euro 2024. AFP – JAVIER SORIANO

Olimpiki za Paris 2024: Sherehe ya Ubora wa Kimichezo

Olimpiki za Paris iliangaza majira ya joto kwa matukio ya kusisimua. Rekodi zilivunjwa, na mashujaa walijitokeza katika michezo tofauti kuanzia kwenye soka, riadha, ngumi, voliboli, basketiboli na michezo mingine mingi.

Wapenzi wa riadha kutoka bara Afrika wakiusherehekea ushindi wa wanariadha kutoka barani Afrika Letsile Tebogo kutoka Botswana, Faith Kipyegon kutoka kenya, Gudaf Tsegay, Tamirat Tola kutoka Ethiopia na Joshua Cheptegei raia wa Uganda.

La Kényane Faith Kipyegon exulte après sa troisième médaille d'or olympique sur 1 500m, le 10 août 2024, lors des Jeux de Paris au Stade de France.
La Kényane Faith Kipyegon exulte après sa troisième médaille d’or olympique sur 1 500m, le 10 août 2024, lors des Jeux de Paris au Stade de France. AP – Matthias Schrader

Ndondi za Uzito wa Juu: Usyk Dhidi ya Fury

Mapambano ya ndondi yamekua mengi mwaka huu. Si Afrika Mashariki, si kusini mwa Afrika, si kaskazini mwa Afrika na duniani kote ila pambano la uzani wa juu lake Oleksander Usyk na Tyson Fury limechukua nafasi kubwa.

Oleksandr Usyk alithibitisha ubora wake kama mmoja wa mabondia wakubwa wa kizazi hiki kwa mara nyingine baada ya kumshinda Tyson Fury kwa pointi katika marudiano yao yaliyofanyika Riyadh, Saudi Arabia. Kwa ushindi huu wa 116-112 kutoka kwa majaji wote watatu, Usyk alidumisha mikanda yake ya WBA (Super), WBC, na WBO na kupanua rekodi yake ya kutoshindwa hadi ushindi 23 wa kulipwa.

Oleksandr Usyk et Tyson Fury pendant la conférence de presse, le 19 décembre 2024 à Riyad, Arabie saoudite.
Oleksandr Usyk et Tyson Fury pendant la conférence de presse, le 19 décembre 2024 à Riyad, Arabie saoudite. Action Images via Reuters – Andrew Couldridge

Ligi ya Mabingwa CAF na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake.

Soka la vilabu barani Afrika lilipanda kiwango mwaka huu, kwa kampeni za kusisimua kwenye Ligi ya Mabingwa ya CAF na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.

Al Ahly SC, klabu ya soka ya Misri, ilifanikiwa kuongeza rekodi ya taji lao la 12 la Ligi ya Mabingwa wa CAF mnamo 2024. Walifanikisha hili kwa kuishinda Espérance de Tunis kwa jumla ya bao 1-0 kwenye fainali.

Ushindi huu uliimarisha zaidi ubabe wa Al Ahly katika soka la vilabu barani Afrika.

Katika mashindano ya kinadada ambayo ufanyika kwa mtindo tofauti na mashindano ya wanaume klabu ya Tp Mazembe ya kinadada iliibuka na ushindi.

Le TP Mazembe a remporté sa première Ligue des champions féminine de la CAF.
Le TP Mazembe a remporté sa première Ligue des champions féminine de la CAF. AFP – ANNE-CHRISTINE POUJOULAT

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment