Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mjumbe wa Jumuiya ya nchi za IGAD Lawrence Korbandy anatarajiwa kuzuru nchini Sudan mwezi Januari kujaribu kusuluhisha mzozo unaoendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF ambao wamekuwa wakipigana tangu mwezi Aprili mwaka 2023.

Jitihada hizi za usuluhishi zinatarajiwa kufanyika wakati Sudan na uhusiano baridi na Jumuiya ya IGAD ambayo iliisimamisha uanachama kutokana na vita vinavyoendelea.
Mjumbe huyo atarejea Sudan, baada ya jitihada za hapo awali zilizoongozwa na IGAD, Marekani na Saudi Arabia kujaribu kuwaleta Majenerali Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza RSF na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan kwenye meza ya mazungumzo, kugonga mwamba.
Mwezi Januari, IGAD ilialika pande mbili zinazozana kwenye kikao cha pamoja jijini Kampala, lakini mkutano huo haukufanyika baada ya uongozi wa kijeshi kudai kuwa Jumuiya hiyo ilikuwa inaingia mambo yake ya ndani.
Korbandy amesema anatumai kuwa ziara yake itasaidia kumaliza vuta hivyo ambavyo vimesabisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha wengine zaidi ya Milioni 12 kuyakimbia makaazi yao.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.