Urusi yatangaza kubadilishana askari wafungwa 300 wa Urusi na Ukraine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa upatanishi wa Falme za Kiarabu, Moscow na Kyiv zimekubali kubadilishana wanajeshi 150 waliotekwa kutoka kila kambi siku ya Jumatatu, kwa jumla ya wanajeshi 300 wa Urusi na Ukraine, kulingana na Urusi. Ukraine, kwa upande wake, imeripotiaskari 189 wamerejea nyumbani kutoka Urusi baada ya kuachiliwa.

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika uwanja wa vita karibu na mji wa Toretsk, huku kukiwa na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, katka jimbo la Donetsk, Ukraine tarehe 20 Desemba 2024.
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika uwanja wa vita karibu na mji wa Toretsk, huku kukiwa na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, katka jimbo la Donetsk, Ukraine tarehe 20 Desemba 2024. REUTERS – Stringer

Urusi imetangaza Jumatatu, Desemba 30, kuwa imebadilisana na Ukraine wanajeshi wafungwa 150 kutoka kila kambi hizo mbili, kufuatia upatanishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu na inapo karibia Sikukuu ya mwaka mpya.

“Mnamo Desemba 30, kufuatia mchakato wa mazungumzo, wanajeshi 150 wa Urusi wamerejeshwa nyumbani kutoka eneo lililodhibitiwa na serikali ya Kyiv Kwa kubadilishana wafungwa. Wafungwa 150 wa jeshi la Ukraine wamekabidhiwa,” jeshi la Urusi limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kwa upande wake, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amehakikisha kwamba raia 189 wa Ukraine wameachiliwa kwa jumla, wakiwemo wanajeshi na raia wawili, “habari njema sana”. Urusi, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, iliripoti tu Waukraine 150 walioachiliwa na Moscow.

Falme za Kiarabu yapongezwa kwa kazi iliyofanya

Kulingana na jeshi la Urusi, “Falme za Kiarabu umetoa upatanishi wa kibinadamu kwa kurudi kutoka kwa mateka ya wanajeshi wa Urusi”, ambao “kwa sasa wako” huko Belarusi, mshirika wa Moscow na jirani wa Ukraine.

Umoja wa Falme za Kiarabu, ambao unashiriki sana katika majadiliano juu ya kubadilishana wafungwa kati ya Kyiv na Moscow, pia hutumika kama mpatanishi wa kurejeshwa kwa watoto wa Ukraine nchini mwao kutoka Urusi.

Mchunguzi wa haki za binadamu wa Urusi Tatiana Moskalkova amekaribisha kwenye Telegram “ujasiri” wa wanajeshi wa Urusi walioachiliwa huru, wakati wa mazungumzo mafupi nao yaliyotangazwa kwenye video kwenye kituo chake cha Telegram. “Heri ya Mwaka Mpya!”, Almengeza, akiwatakia “kila la kheri”.

Urusi na Ukraine zimebadilishana mamia ya wafungwa tangu mashambulizi ya Urusi kuanza mwezi wa Februari 2022 na kubadilishana mara kwa mara mabaki ya wanajeshi waliouawa kwenye mapigano hayo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment