Jinsi Mungu anavyojitukuza,Unaona nini mbele ya magumu yako?

Mungu hakumzuia Farao kuwafata wana wa Israel walipotoka Misri tena aliufanya moyo wake kuwa mgumu kabisa ili asikate tamaa ya kuwafatilia lakini alikua na maana yake,alimpiga pigo ambalo mpaka leo ni historia aliangamiza majeshi yake na siraha na magari na farasi ndani ya bahari ya shamu,hata wewe ambaye unaona adui yako amekazana sana kukufatilia maisha yako kila ukiomba mashambulizi ndio yanazidi usiogope kama Musa alivyo waambia wana wa Israel hawa wa Misri mnaowaona leo hamtawaona tena ndivyo na mimi nakwambia hao adui unaowaona leo,hayo mateso unayopitia leo,hizo shida masengenyo na dharau unazo zipata leo hutazipata wala kuziona tena hili ni neno la Mungu linakuijia leo.
Mungu anamfanya adui yako asikate tamaa ya kukufata ili aje hampige na kumuangamiza kabisa na watu wote watamsujudia Mungu wako.Hiyo ndiyo Tabia ya Mungu Usiogope.
Kifo, kushindwa, kukata tamaa, kufungwa, kufukuzwa, kuachwa, kuzirai, kufeli?
Kama unaona hivyo jua kuwa hicho ndicho kitu halisi kinachokuumiza WALA SIO TATIZO UNALOHISI LINAKUUMIZA.
Habari njema kwako ni ushauri huu.
Acha kutazama hayo, MTAZAME BWANA ndipo utaona anakuonyesha jambo jema na nzuri ndani ya hilohilo tatizo unaloliogopa sana.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment