Mgogoro nchini Msumbiji: Afrika Kusini yateua mjumbe maalum

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Afrika Kusini imemteua mjumbe maalum, Sydney Mufamadi, kujaribu kurejesha hali ya utulivu katika nchi jirani ya Msumbiji. Nchi imetikiswa na maandamano ya vurugu tangu kuchaguliwa kama mkuu wa nchi mnamo Oktoba 9, 2024 mgombea wa Frelimo, chama kinachotawala kwa miaka 50. Wiki iliyopita, kuthibitishwa kwa ushindi huu na mahakama ya juu zaidi nchini kulizua ghasia.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia amemteua mshauri wake wa masuala ya usalama - Sydney Mufamadi - mjumbe maalum nchini Msumbiji kuzungumza na washikadau na kujaribu kurejesha utulivu.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia amemteua mshauri wake wa masuala ya usalama – Sydney Mufamadi – mjumbe maalum nchini Msumbiji kuzungumza na washikadau na kujaribu kurejesha utulivu. © URS FLUEELER / AFP

Maandamano ya vurugu, ghasia za mijini, uharibifu, uporaji na maelfu ya raia wa Msumbiji waliokimbia nchi. Afrika Kusini ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea kwa machafuko katika eneo hilo. Kutoroka kwa zaidi ya wafungwa elfu moja katika gereza lenye ulinzi mkali katika mji mkuu wa Msumbiji wiki iliyopita kumechangia hali ya ukosefu wa usalama nchini humo.

Kulingana na mamlaka, zaidi ya raia 10,000 wa Msumbiji wameikimbia nchi katika siku za hivi karibuni na kukimbilia Malawi.

Afrika Kusini imetangaza kuwa imeimarisha operesheni zake za pamoja na jirani yake kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili ili kuzuia uhalifu unaoweza kujitokeza kufuatia machafuko hayo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pia amemteua mshauri wake wa masuala ya usalama – Sydney Mufamadi – mjumbe maalum nchini Msumbiji kuzungumza na washikadau na kujaribu kurejesha utulivu.

Na hii wakati upinzani, ambao unaendelea kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais, umeonyesha kuanzishwa kwa maandamano wiki hii. Takriban watu 134 walikufa katika siku chache.

Rais mteule Daniel Chapo anatarajiwa kuingia madarakani ndani ya wiki mbili.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment