Korea Kusini: Mahakama yatoa hati ya kukamatwa kwa rais aliyetimuliwa Yoon

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama ya Korea Kusini imetoa kibali cha kukamatwa kwa Rais aliyepinduliwa Yoon Suk Yeol kwa jaribio lake lisilofanikiwa la kuweka sheria ya kijeshi mapema mwezi huu, wachunguzi wanaosimamia uchunguzi wamesema siku ya Jumanne.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati wa hotuba yake kwenye televisheni tarehe 3 Desemba 2024.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol wakati wa hotuba yake kwenye televisheni tarehe 3 Desemba 2024. © South Korea Unification Ministry via AP

“Waranti ya kukamatwa na hati ya upekuzi dhidi ya rais Yoon Suk-yeol… imetolewa asubuhi ya leo,” mamlaka inayoongoza uchunguzi wa pamoja dhidi ya Yoon Suk-yeol imesema katika taarifa. “Hakuna ratiba iliyoanzishwa kwa ajili ya kuendelea na taratibu,” imeongeza.

“Hati ya kukamatwa na hati ya upekuzi na kukamata iliyotolewa kwa ombi la taasisi ambayo haina mamlaka ya uchunguzi ni kinyume cha sheria na ni batili,” ameshutumu Yoon Kab-keun, wakili wa Yoon Suk-yeol, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Korea Kusini kwa rais aliyeko madarakani kulengwa na hatua hizo za kisheria, huku Yoon Suk-yeol akiwa bado yuko madarakani akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba kuhusu kufutwa kwake kazi, hatu iliyopitishwa Desemba 14 na Bunge la taifa .

Kwa sasa amesimamishwa kazi, huku Mahakama ikitarajiwa kuthibitisha au kutengua kufukuzwa kwake katikati mwa mwezi wa Juni.

Yoon Suk-yeol aliishangaza nchi mnamo Desemba 3 kwa kutangaza sheria ya kijeshi kwa mshangao na kutuma jeshi Bungeni kuzuia kuidhinisha hatua yoyote. Alilazimika kurejelea hatua yake saa chache baadaye chini ya shinikizo kutoka kwa wabungena maelfu ya waandamanaji waliokuwa wameingia mitaani.

Anachunguzwa, haswa kwa “uasi”, uhalifu ambao kinadharia unaweza kuadhibiwa na kifo, na haruhusiwi kuondoka nchini.

Kukataa kutii

Mwendesha mashtaka nyota wa zamani mwenye umri wa miaka 64 alikataa mara tatu kutii wito wa kuhojiwa kuhusu mapinduzi yake, na kusababisha ombi la kukamatwa kwake siku ya Jumatatu.

Afisa kutoka ofisi ya cheo cha juu ya uchunguzi wa ufisadi alitaja kukataa mara kwa mara kwa Yoon Suk-yeol siku ya Jumanne kumehalalisha ombi hili. “Waraka huo ni halali hadi Januari 6 [Jumatatu asubuhi],” amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari, akibainisha kwamba rais aliyeondolewa anaweza kupelekwa kituo cha polisi au katika kituo cha kizuizini cha Seoul.

Hata kama hati ya kukamatwa imetolewa, hakuna uhakika kwamba mamlaka itaweza kumkamata Yoon Suk Yeol, huduma zake za usalama tayari zimezuia upekuzi mara tatu, ingawa kwa kibali.

Kiosi cha walinzi wa rais, kwa upande wake, kimehakikisha kwamba kitachukuwa hatua “kwa kufuata taratibu za kisheria”, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa vyombo vya habari vya ndani.

Polisi wametumwa nje ya makazi ya Bw. Yoon katikati mwa Seoul, kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP kwenye eneo la tukio. Waandamanaji wanaodai aondolewe bila shaka na wengine wanaomuunga mkono pia wapo, vyombo vya habari vikirusha picha za makabiliano kati ya kambi hizo mbili yalizotokea usiku.

Kitaalamu, yeyote anayepinga kutekelezwa kwa hati ya kukamatwa anaweza kukamatwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment