Korea Kusini: Takriban watu 160 wafariki katika ajali ya ndege iliyobeba watu 181

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Jeju Air imepoteza muelekeo kwenye njia ya kurukia na kuanguka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan, Korea Kusini, na kuua takriban watu 160, Jumapili, Desemba 29, 2024. Mkuu wa shirika la ndege la Jeju Air ameomba msamaha za kampuni kwa familia wa wahanga.

Wafanyakazi wa uokoaji na wazima moto karibu na ajali ya ndege iliyowasili kutoka Bangkok, Thailand na kutua Muan, Korea Kusini, Desemba 29, 2024.
Wafanyakazi wa uokoaji na wazima moto karibu na ajali ya ndege iliyowasili kutoka Bangkok, Thailand na kutua Muan, Korea Kusini, Desemba 29, 2024. © Maeng Dae-hwan / AP

Ajali hiyo imetokea wakati ndege ya shirika la ndege la Jeju Air ikitua kutoka Bangkok, Thailand, ikiwa na abiria 175 na wafanyakazi sita. Uwanja wa ndege wa Muan uko kusini mwa Korea Kusini.

Ndege hiyo “imeharibika kabisa” na abiria na wafanyakazi walikuwa na “nafasi ndogo ya kunusurika,” wazima moto kwenye eneo la tukio wamesema. Kadiri saa zilivyosonga mbele, hali ilizidi kuwa mbaya, hivyo kuthibitisha kukata tamaa kwa maafisa wa kikosi cha zima moto waliofika eneo hilo ambao walikuwa wametaja idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa vibaya.

Kiongozi wa shirika la ndege la Jeju Air ameomba msamaha kwa niaba yake na kwa niaba ya shirika analoongoza kwa familia za abiria.

Awali ya yote, ningependa kuinama na kuomba msamaha kwa kila mtu anayethamini shirika la ndege la Jeju Air. Zaidi ya yote, napenda kutoa pole na pole kwa abiria na familia zao waliopoteza maisha katika ajali hii. Kwa sasa ni vigumu kubaini chanzo cha ajali hiyo, na ni lazima tusubiri uchunguzi rasmi na tangazo kutoka kwa vyombo husika vya serikali. Haijalishi ni sababu gani ya ajali, ninahisi kuwajibika kama Mkurugenzi Mtendaji. Jeju Air, tutafanya tuwezavyo ili kutatua tatizo la ajali kwa haraka na kusaidia familia za abiria. Pia tutajitahidi kubaini chanzo cha ajali hiyo kwa kushirikiana na serikali. Kwa mara nyingine tena, naziombea roho za waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kutoa pole za dhati kwa familia zilizofiwa.

“Uchunguzi utafafanua kwa usahihi sababu za ajali”, amesema mkuu wa shirika la ndege la Jaju Air.

Kwa mujibu wa habari za awali, ndege hiyo ilijaribu kutua kwa mara ya kwanza mwendo wa saa 3:00 asubuhi kwa saa za huko. Lakini hitilafu ya gia ya kutua ilionekana kuzuwia kitendo hiki, anaripoti mwandishi wetu wa Seoul, Camille Ruiz. Kwa hivyo marubani walijaribu kutua ghafla. Katika jaribio la pili, ndege hiyo iliondoka kwenye njia ya kurukia kwa mwendo wa kasi na kugonga ukuta wa uwanja wa ndege kabla ya kuwaka moto.

 Wizara ya Nchi, iliynukuliwa na shirika la habari la AFP, inabainisha kuwa ndege hiyo ilikuwa imetoa ujumbe wa dhiki baada ya jaribio la kwanza la kutua, ambapo maafisa kweye uwanja wa ndege wliwaonya wafanyakazi kwamba ndege hiyo iligonga ndege waliokuwa wakiruka. Video iliyorushwa na shirika la utangazaji la Korea Kusini MBC inaonyesha ndege hiyo ikitua na moshi kutoka kwa injini, bila gia ya kutua. Ndege hiyo inatoka kwenye njia ya kurukia na kuvamiwa na moto.

Takriban wanajeshi 180, magari ya zima moto na magari ya kubebea wagonjwa yametumwa haraka kwenye eneo hilo kudhibiti moto huo na kuwatoa abiria.

Kulingana na tovuti maalum ya Flightradar, ndege hiyo ni Boeing 737-8AS kutoka shirika la ndege la low cost la Korea Kusini Jeju Air, ambayo ilianza kuhudumu mnamo Agosti 2009. Ndege hiyo ilikuwa ikirejea kutoka Bangkok. Ilikuwa na watu 181. Wengi ni Wakorea, wawili ni raia wa Thailand. Kulingana na mamlaka, wanawake wawili waliokolewa, wafanyakazi wawili walitolewa muda mfupi baada ya ajali. Walipelekwa hospitali.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment