Korea Kusini: Wachunguzi watafuta kibali cha kukamatwa kwa rais aliyetimuliwa Yoon

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wachunguzi wa Korea Kusini wamesema siku ya Jumatatu Desemba 30 wameiomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa rais aliyen’atuliwa madarakani Yoon Suk-yeol kwa jaribio lake lisilofanikiwa la kuweka sheria ya kijeshi, ambayo iliiingiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akitoa hotuba kwa taifa katika Ikulu ya Rais mjini Seoul, Korea Kusini, Desemba 12, 2024.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akitoa hotuba kwa taifa katika Ikulu ya Rais mjini Seoul, Korea Kusini, Desemba 12, 2024. via REUTERS – Korean Presidential Office

Siku moja baada ya kukataa kwa mara ya tatu kwa Yoon Suk-yeol kufika kuhojiwa, huduma za uchunguzi ziliwasilisha ombi lao kwa mahakama ya Seoul, wamesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Alipofutwa kazi na Bunge mnamo Desemba 14, Yoon Suk-yeol kwa sasa amesimamishwa kazi akisubiri Mahakama ya Kikatiba kuthibitisha au la uamuzi wa wabunge hao, na amepigwa marufuku kuondoka nchini.

Yeye ndiye mlengwa wa uchunguzi wa “uasi”, uhalifu unaostahili adhabu ya kifo, kwa kuweka sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3 na kutuma jeshi kwenye Bunge kujaribu kushinikiza bunge kutochukuwa uamuzi wowote, kabla ya kurejelea hatua yake saa chache baadaye chini ya shinikizo kutoka wabunge na raia waliovamia mitaa na kuandamana.

Kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini, Yoon Suk-yeol, 64, pia anakataa kukiri kupokea wito aliotumwa na Mahakama ya Kikatiba, ambayo ilifanya usikilizwaji wa kwanza wa kesi yake siku ya Ijumaa. Mahakama ina miezi sita kuthibitisha au kutengua hatua ya kumng’atua rais. Ikiwa itachagua suluhu la kwanza, itabidi uchaguzi wa urais ufanyike ndani ya miezi miwili.

Rais aliyechukuwa nafasi yake pia aaondolewa mamlakani

Kwa upande wa kisiasa, rais wa mpito aliyekuwepo tangu katikati ya mwezi wa Desemba, Waziri Mkuu Han Duck-soo, naye alifutwa kazi siku ya Ijumaa, huku wabunge wakimtuhumu kwa kujaribu kuzuia uchunguzi wa mtangulizi wake.

Mkuu mpya wa serikali wa muda, Waziri wa Fedha Choi Sang-mok, ameahidi “kukomesha mgogoro wa serikali”, ambao haujawahi kutokea kwa nchi hii ya nne yenye uchumi mkubwa barani Asia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment