Nimejifunza kushiba na kuona njaa,kuwa na Vingi na kupungukiwa.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.

“Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo MUNGU. Na MUNGU wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya KRISTO YESU. Sasa atukuzwe MUNGU, Baba yetu, milele na milele. Amina.” Wafilipi 4:11-20

Mtumishi;

  1. Hata kama una mahitaji Sana, jifunze kuwa radhi na hali yeyote uliyonayo.

Usiache kumtumikia MUNGU kwa sababu ya mahitaji yako.

  1. Katika Safari yako ya utumishi tambua kwamba kuna kudhiliwa na kuna kufanikiwa.

Kubaliana na hali yeyote utakayo utakayopitia, ila hali hiyo isikufanye upunguze kumtumikia Bwana YESU KRISTO.

  1. Jifunze kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

Wakati wa njaa usidhani MUNGU amekuacha kama weww unamtumikia KRISTO kwa uaminifu bali endelea mbele na utumishi maana kuna wakati wa kufanikiwa pia.

  1. Hakikisha unayaweza mambo yote katika MUNGU akutiaye nguvu.
  2. MUNGU akikuinulia watu ili kukubariki kwa matoleo yao basi waombee sana waru hai na wabariki sana mbele za MUNGU ili wafanikiwe katika maisha yao yote.

Waombee ili kutoa kwao sadaka, Dhabihu na zaka, huko kutoa kulete kupokea sana kutoka kwa MUNGU.

MUNGU akubariki kwa kujifunza ujumbe huu.

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment