Rais anayeondoka Zoran Milanovic na mpinzani wake Dragan Primorac waingia duru ya pili

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais anayemaliza muda wake Zoran Milanovic ambaye awali alipewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza, hatimaye atamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais na mpinzani wake wa kihafidhina, Dragan Primorac, kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa siku ya Jumapili, Desemba 29 na Tume ya Uchaguzi.

Rais wa Croatia anayemaliza muda wake Zoran Milanovic amefuzu kuingia duru ya pili kwa 49.20% ya kura, akifuatiwa na Dragan Primorac aliyepata 19.43% ya kura, Jumapili Desemba 29, 2024.
Rais wa Croatia anayemaliza muda wake Zoran Milanovic amefuzu kuingia duru ya pili kwa 49.20% ya kura, akifuatiwa na Dragan Primorac aliyepata 19.43% ya kura, Jumapili Desemba 29, 2024. © Antonio Bronic, Djordje Kojadinovic Reuters / Montage RFI

Rais wa Croatia anayemaliza muda wake, Zoran Milanovic, kwa asilimia 49.11 ya kura, amekosa kura nyingi. Atalazimika kukabiliana na mhafidhina Dragan Primorac, ambaye amepata 19.37% ya kura, Tume ya Uchaguzi imetangaza siku ya Jumapili, Desemba 29. Kwa kumshinda mpinzani wake kwa kura nyingi hizi, inaonekana kuwa ngumu kwa Milanovic kukosa kupata ushindi katika duru ya pili itakayofanyika Januari 12, anabainisha mwandishi wetu wa kikanda, Laurent Rouy.

Kwa mshangao wa kila mtu, uchunguzi wa kura ya maoni kutoka taasisi ya IPSOS, ilimpa rais anayemaliza muda wakeushindi katika duru ya kwanza. Katika uchunguzi wa kura ya maoni, IPSOS ilimtaja Zoran Milanovic msindi kwa 51.48% ya kura, ikilinganishwa na 19.29% ya mpinzani wake.

Kushinda kwa Waziri Mkuu wa sasa

Matokeo yake ni ya kushangaza, kwa sababu katika uchaguzi wa wabunge mwezi Aprili, Wacroatia walipiga kura kuunga mkono chama cha kihistoria cha kihafidhina cha HDZ, kilekile kilichomuunga mkono Dragan Primorac, kumzuia Milanovic ambaye alitaka kuwa Waziri Mkuu.

Katika miezi ya hivi karibuni, maisha ya kisiasa ya Croatia yamekuwa na majibizano ya maneno kati ya Rais Milanovic na Waziri Mkuu Andrej Plenkovic, haswa juu ya uungaji mkono wa Ukraine kwenye vita. Milanovic analaani uchokozi wa Urusi lakini anakosoa misaada ya Magharibi, ambayo imesababisha ashtumwe kuwa anaunga mkono Urusi. Croatia bado ilituma msaada wa kijeshi kwa Ukraine kiasi cha euro milioni 300.

Wacroatia walipiga kura siku ya Jumapili kwa idadi ndogo sana kuliko katika uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Aprili. Ushiriki, kwa kuzingatia idadi sawa ya kura zilizohesabiwa, ulikuwa 46%, ikilinganishwa na 62% katika uchaguzi wa wabunge. Zaidi ya 51% ya wapiga kura walipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2019. Ushiriki huu mdogo unaweza kuelezewa na tarehe ya uchaguzi, kati ya Krismasi na Mwaka Mpya, wakati watu wengi wako likizo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment