Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mwandishi wa habari wa Italia, Cecilia Sala, ambaye alikuwa nchini Iran kama sehemu ya kazi yake, alikamatwa mnamo Desemba 19 na polisi wa Tehran, Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia imetangaza siku ya Ijumaa Desemba 27, 2024.

Ubalozi wa Italia na ubalozi mdogo mjini Tehran unafuatilia kesi ya mwandishi huyo wa habari na balozi wa Roma nchini Iran, Paola Amadei, amemtembelea leo kuangalia mazingira ambamo anazuiliwai, imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Gazeti la kila siku la La Repubblica, mwanahabari huyo alikuwa nchini Iran kwa takriban siku kumi na alikuwa akijiandaa kurejea Italia alipokamatwa.
Aliwasili Iran kwa visa ya mwandishi wa habari na kuchapisha ripoti kadhaa kuhusu mabadiliko katika nchi hii baada ya kuanguka kwa Rais Bashar Al Assad nchini Syria, kulingana na chanzo hicho.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.