Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Gabon, Alain-Claude Bilie-By-Nze, mpinzani mkuu wa utawala wa kijeshi ulioko madarakani, ametembelea ikulu ya rais siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza. Alimpa mkono Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema, afisa mkuu wa jeshi aliyevunja serikali yake mwaka wa 2023. Waziri mkuu huyo wa zamani alikuja kumpa mkuu wa nchi waraka uliokuwa na mapendekezo yake ya kujondokana kwenye mpito wa kisiasa.

Nchini Gabon, ishara ya utulivu wa kisiasa. Alain-Claude Bilie-By-Nze aliondoa chumvi kwenye donda kwa kukutana na rais wa mpito siku ya Ijumaa, Desemba 27. Waziri Mkuu wa mwisho wa Ali Bongo Ondimba alimpa mkono Brice Clotaire Oligui Nguema, jenerali aliyevunja serikali yake zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mwishoni mwa mkutano huo, Alain-Claude Bilie-By-Nze alisema amekuja Ikulu ya rais kumkabidhi rais wa mpito, Brice Clotaire Oligui Nguema, mapendekezo yaliyotengenezwa na jukwaa lake la kisiasa, kwa jina la Ensemble pour Gabon. Lengo lililotajwa ni kuhakikisha uwazi wa uchaguzi ambao utakomesha mpito wa sasa.
Waziri Mkuu wa mwisho wa Ali Bongo, ambaye alikuja kuwa mmoja wa watu waliotoa sauti kali dhidi ya wanajeshi waliokuwa madarakani, alipendekeza kwamba Kanuni ya Uchaguzi, ambayo inafanyiwa marekebisho hivi sasa, iondoe utaratibu wa uchaguzi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuunga mkono tume huru ya uchaguzi. Pia alitoa wito wa kufanyiwa marekebisho upya faili la uchaguzi lililorithiwa kutoka kwa serikali iliyoanguka pamoja na mgawanyiko mpya wa uchaguzi.
Jukwaa la Alain-Claude Bilie-By-Nze pia lilimwomba Rais Oligui Nguéma kufadhili na kufidia gharama za kampeni. Sharti la mwisho: kuchapishwa kwa kalenda ya uchaguzi ambayo itamaliza mpito. Kulingana na ratiba ya awali iliyochapishwa na jeshi, kipindi cha mpito kinapaswa kumalizika mwei Agosti mwaka ujayo. Nchi lazima ndani ya tarehe hii ya mwisho kuandaa, kwa utaratibu ambao bado haujawasilishwa, uchaguzi wa rais, uchaguzi wa wabunge na uchaguzi wa serikali za mitaa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.