Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Tangu mwaka 2011, Syria imekuwa ikikabiliwa na tatizo la nishati. Migogoro imeharibu miundombinu, na kupunguza upatikanaji wa umeme na gesi. Leo, huko Damascus, nyumba zina saa mbili tu za umeme kwa siku, na mitungi ya gesi, nadra na ya gharama kubwa, inashindwa kukidhi mahitaji ya kimsingi.

Katika mji wa Jaramana, ulio katika kitongoji cha kusini mashariki mwa Damascus, Saeed, 40, anaishi katika ghorofa iliyo na vifaa vya kutosha: vigae visivyo na doa, oveni, jokofu, mashine ya kuosha. Lakini hakuna kitu kinachofanya kazi: bila gesi au umeme, hakuna kinachoendelea.
Kukosekana kwa umele au gesi huacha familia yake kwenye baridi na giza, na kulazimisha kila mtu kujikongoja kwa maisha ya kila siku. “Hatuwezi kuweka chakula kwenye friji kwa sababu kinaharibika, hatuwezi kujaza maji kwenye tanki zetu za juu, na hatuwezi kuwaacha watoto waoge maji ya baridi kwa sababu maji hayawezi kupashwa moto. Kusema ukweli tatizo hili tunateseka sana na tunatarajia Mungu atatutatulia tatizo hili ili tuishi maisha ya kawaida,” anasema baba huyo.
Sio mbali na nyumba ya Saeed, Haitham, mwenye duka kubwa, anajitahidi kuhifadhi bidhaa zake. Friji zake zinawashwa kwa kutumia jenereta ya petroli, anasa ya gharama kubwa. Kutokana na gharama kubwa, amepunguza saa zake za kazi na kunahatari ya kufunga kabisa duka lake.
“Umeme unapatikana kuanzia saa 6 mchana hadi saa 7 mchana, kisha unakatika hadi saa 12 jioni, kisha unarudi kwa saa moja na unakata tena hadi usiku wa manane, saa 7 usiku unarejeshwa kwa dakika kadhaa, halafu unakata. Bidhaa zinaharibika haraka dukani, hatununui bidhaa nyingi, lakini tu tunazoweza kuuza kwa wakati,” anaelezea Haitham.
Serikali ya mpito inaahidi uboreshaji kutokana na makubaliano na Jordan na Uturuki ya kuunganisha tena Syria kwenye gridi ya nishati. Wakati wakisubiri matokeo ya ahadi hizi, Wasyria wanasalia kuwa wafungwa wa maisha ya kila siku ambapo mwanga na joto vimekuwa haki adimu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.