Chad: Saleh Déby Itno, baba mdogo wa Mahamat Idriss Déby afariki dunia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Saleh Deby Itno amefariki siku ya Jumanne, Desemba 24. Kaka mdogo wa Idriss Deby na baba mdogo wa mkuu wa nchi wa sasa, amefariki kufuatia “ugonjwa wa muda mfupi” huko Misri ambapo alikuwa akisafirishwa kufanyiwa matibabu, kulingana na watu wa familia yake walionukuliwa na vyombo vya habari vya Chad. 

Saleh Déby Itno alijiunga na chama cha upinzani cha Socialist Party Without Borders (PSF), akiwa mmiliki wa (jengo) makao makuu ya chama hiki. Hapa, jengo husika, ambalo liliharibiwa wakati wa operesheni na mamlaka, huko Ndjamena.
Saleh Déby Itno alijiunga na chama cha upinzani cha Socialist Party Without Borders (PSF), akiwa mmiliki wa (jengo) makao makuu ya chama hiki. Hapa, jengo husika, ambalo liliharibiwa wakati wa operesheni na mamlaka, huko Ndjamena. © François Mazet/RFI

Akiwa ameshikilia nyadhifa kadhaa serikalini, alijulikana kwa uhusiano wake tata na kaka yake wakati huo na mtoto wa kaka yake, rais wa sasa wa Mpito Idriss Deby Itno. Hivi karibuni alijiunga na upinzani.

Kwa mujibu wa watu wa familia yake waliowasiliana na vyombo vya habari vya Chad, Saleh Déby amefariki nchini Misri ambapo ndege iliyombeba ilitua kwa dharura alipokuwa akipelekwa Paris kwa matibabu. Haya yanathibitishwa na chanzo chenye ufahamu mkubwa, ambacho kinahakikisha kuwa ni ofisi ya rais ndio iliokodi ndege hiyo.

Kuhusu sababu za kifo, vyanzo hivi vinataja “ugonjwa wa muda mfupi” bila kutoa maelezo. Wanaibaini afya dhaifu ya Saleh Déby, na hali ambayo imezorota katika miezi ya hivi karibuni.

Mwanzoni mwa mwaka 2024, alijiunga na upinzani na alikamatwa wakati wa shambulio dhidi ya makao makuu ya PSF, ambalo liligharimu maisha ya Yaya Dilo mwishoni mwa mwezi wa Februari. Kisha aliachiliwa mnamo mwezi Aprili.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment