Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani leo Jumatano, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo wakati dunia ikielekeza macho yake katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina,  katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina na Syria.

Sikukuu ya Krismasi 2020.
Sikukuu ya Krismasi 2020. Church of England

Mamia ya watu walikusanyika katika kanisa la Uzawa katika mji mtakatifu kwa Wakristo wa Bethlehem Jumanne kuadhimisha Krismasi nyingine iliyogubikwa na vita katika Ukanda wa Gaza.

Wakristo duniani kote wanamiminika Makanisani hii leo kuadhimisha siku kuu ya Krismasi. Kulingana na imani ya Kikristo, Krismasi ni siku kuu ambayo wanaamini kuwa Yesu Kristo (Isa) alizaliwa bethlehemu nchini israeli.  Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.

Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.

Mjini Bethlehem nchini Israel, mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, mwaka huu hakukushuhudiwa shamrashamra kama miaka ya nyuma kutoka na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas, huku wengine wakiendelea kuandamana kwa kutaka ndugu zao wanaoshikilia na kundi hili la wanamgambo wa Hamas waachiliwe mara moja na Israel ikomeshe vita vyake dhidi ya raia wa Palestina.

Kihistoria, Bethlehem huangazwa na mti mkubwa wa Krismasi katika Uwanja wa Manger, lakini kwa mwaka wa pili mfululizo, mamlaka za eneo hilo zilichagua kutoandaa sherehe kubwa. 

Katika ujumbe kwa Wakristo ulimwenguni kote, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu aliwashukuru kwa kuunga mkono mapambano ya Israel dhidi ya “nguvu za uovu.” 

“Mmekuwa upande wetu kwa uthabiti, wakati wote na kwa nguvu wakati Israel inatetea ustaarabu wetu dhidi ya unyama,” alisema.

 All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment