Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wakuu wa kitengo cha Inteljensia kutoka Ethiopia na Somalia; wamekutana jijini Addis Ababa, kujadili ushirikiano kuhusu masuala ya ulinzi na usalama, baada ya makubaliano ya Ankara yaliyotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mapema mwezi huu.

Mazungumzo hayo yameongozwa na Mkuu wa Inteljensia kutoka Ethiopia Redwan Hussien, ambaye amekuwa mwenyeji wa mgeni wake Abdullahi Mohamed Ali, ambao baada ya mazungumzo yao yaliyojikita katika ushirikiano na utatuzi wa changamoto zinaziwakabili kwa pamoja.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa X, Hussien amesema kuwa mazungumzo hayo ya ushirikiano yataendelea bila kujali maadui wa ndani na nje wa nchi zao.
Wawili hao wamekutana wakati ujumbe mwingine wa Somalia, ukiongozwa na Waziri wake wa Mambo ya nje na Ushiriakino wa Kimataifa Ali Omar,kuwasili jijini Addis, kukutana na mwenyeji wake, ili kuendelea kutekeleza makubaliano ya Ankara.
Desemba tarehe 12, mataifa hayo mawili, yalitia saini mkataba wa kusisitisha mvutano kati yao, baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland kuhusu matumizi ya Bahari, jambo ambalo liliikarisha utawala wa Mogadishu.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, walikuliana kutatua tofauti zao kwa njia ya mazungumzo huku kila upande ukiheshimiana
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.