DRC: Askofu Mkuu wa Kinshasa atoa ujumbe wa Krismasi kwa serikali kuzingatia amani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), askofu mkuu wa Kinshasa Fridolin Ambongo, ametoa wito kwa mamlaka kuhamasisha amani na kukomesha masaibu yanayowapata Wakongo, katika nchi ambayo ameitaja “kuzimu” na ambayo iko katika “janga.”

Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, wakati wa misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Notre-Dame du Kongo mjini Kinshasa, Desemba 24, 2023.
Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, wakati wa misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Notre-Dame du Kongo mjini Kinshasa, Desemba 24, 2023. © PATRICK MEINHARDT / AFP

Kardinali Fridolin Ambongo amezungumza kwa kirefu kuhusu hali nchini humo wakati wa mkesha wa Krismasi katika Kanisa Kuu la Notre Dame du Congo, katika mji mkuu Kinshasa. Miundombinu hakuna, kupanda kwa bei ya bidhaa za msingi, ukosefu wa usalama unaoenea kote nchini… kwake, nchi inaonekana kama “kuzimu duniani”. Huko Kinshasa, anaelezea, watu wametelekezwa na “hajui tena waelekee njia gani”.

Mikoani, masaibu hayaelezeki, anahakikisha Fridolin Ambongo. Wakati wa kusherehekea Krismasi, askofu mkuu anatoa wito kwa mamlaka “kujiuliza”. “Tunatoa wito kwa kila mtu, haswa wale wote walio na jukumu katika nchi hii, kusimama ili masaibu haya yaweze kumalizika. Unapokuwa kiongozi, kwanza unakuwa kwa ajili ya furaha ya wananchi na wananchi wanapokuwa katika hali hii mbaya, iwe changamoto kwa wenye mamlaka. Je, tumefanya nini ili watu wafikie hatua hii? », anabainisha kardinali.

Kuhusu hali ya usalama na kutekwa kwa maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, makundi yenye silaha ambayo bado yanapigana katika mikoa ya mashariki na wanamgambo kwenye malango ya Kinshasa, Kardinali huyo ametaja mikakati ya vita na diplomasia ambayo, kulingana na yeye, “imeonyesha mipaka yao, imeshindwa”. “Nashuhudia hotuba ambazo haziendi katika mwelekeo wa kuleta amani. Ni lazima tufanye kazi kwa ajili ya amani,” anasema Kardinali.

Katika mahubiri yake, kardinali hakurejelea kwenye mjadala kuhusu uwezekano wa mageuzi ya Katiba, yaliyotakwa na Rais Félix Tshisekedi na kupingwa vikali na Kanisa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment