Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Meli ya Urusi yazama kwa mlipuko katika chumba cha injini
- Maandamano yaibuka Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi
- Amorim ahoji ‘chaguo’ za washauri wa Rashford
- Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alazwa hospitalini
- Chombo cha anga za mbali chajaribu kulikaribia jua
- Mke wa mwanasiasa wa Uganda anayezuiliwa Kizza Besigye alaani marufuku ya kumtembelea siku ya Krismasi
- Urusi yakanusha ripoti kwamba mke wa Assad anataka talaka
- Israel yathibitisha kumuua kiongozi wa Hamas Haniyeh mjini Tehran
Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 24/12/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Mashariki mwa DRC: Mapigano ya kudhibiti Lubero yaendelea na maeneo yenye amani yakumbwa vita
Katika mashariki mwa DRC, vita vinaendelea kati waasi wa M23 – wanaoungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) – wakiungwa mkono na wanamgambo wa eneo hilo. Siku ya Jumatatu, Desemba 23, vita viliendelea yakumba maeneo kadhaa katika eneo la Lubero. Wakati huo huo, mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine yaliokuwa katika amani: kuelekea Kibumba, kaskazini mwa Goma, ambapo Cutulivu umetawala kwa wiki kadhaa.

Milipuko ya mabomu na milio ya silaha nzito na nyepesi imesikika kwenye kilima cha Kanadahoro, kwenye barabara inayoelekea Kibumba, karibu kilomita ishirini kutoka Goma: eneo ambalo lilikuwa na utulivu kwa wiki. Risasi za kwanza ziliripotiwa siku ya Jumatatu alasiri.
Kulingana na mashiroka ya kiraia, mapigano pia yayameripotiwa huko Kamatembe, katikati ya Hifadhi ya Virunga.
Mapigano ya mwisho mabaya katika eneo hili yalitokea mapema mwezi Novemba. Kibumba inachukuliwa kuwa ngao kwa ulinzi wa mji wa Goma: miaka miwili iliyopita, M23 ilkubali kujiondoa na kuacha nafasi kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Lakini tangu wakati huo, Majeshi ya DRC (FARDC) hayajawahi kupata udhibiti wa eneo lote.
Kaskazini zaidi, huko Lubero, mapigano mengine yanaendelea, jeshi la Kongo liliendelea mashambulizi yake siku ya Jumatatu. Jumapili, Desemba 22, ilitumia helikopta za kivita na kushambulia ngome za waasi. Lengo: Kujaribu kurejesha kwenye himaya yake eneo la kimkakati la Alimbongo lililoanguka mikononi mwa waasi wa M23 na washirika wake wiki iliyopita, wakati wa mashambulizi makubwa.
Tangu wakati huo, FARDC tayari imechukua udhibiti wa Ndoluma na Mambasa baada ya mapigano makali. Lakini hali inaendelea kuwa tete.
AES yafutilia mbali kipindi cha mpito cha miezi sita kilichopendekezwa na ECOWAS
Mataifa matatu ya Mali, Burkina Faso na Niger yanayoongozwa na jeshi, yamekataa kipindi cha miezi sita kilichotolewa na wakuu wa nchi za kiuchumi za Jumuiya ya ECOWAS, kutafakari iwapo wanataka kurejea kuwa wanachama.
Uamuzi wa nchi hizo, unakuja wiki moja baada ya wakuu wa nchi za ECOWAS waliokutana jijini Abuja nchini Nigeria, kuthibitisha kuwa uamuzi wa Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo, utaanza Januari tarehe 29 mwaka 2025.
Kipindi cha mpito cha miezi sita, kinatoa fursa kwa wakuu hao wa kijeshi kutafakari tena uamuzi wao wa kujiondoa kwenye Jumuiya ya ECOWAS na hata kuwezesha mazungumzpo zaidi kuendelea, lakini wamesisitiza kuwa, hawataki kushiriki kwenye kipindi hicho, wakiishtumu Ufaransa kwa kuwa nyuma ya mpango huo.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa kijeshi wa mataifa hayo matatu, ambayo yameunda jumuiya yao ya Sahel, Kanali Amadou, ambaye ni mshirika wa karibu wa kiongozi wa kijeshi nchini Mali Assimi Goita, amesema mpango huo wa ECOWAS umekataliwa na ni mbinu ya kuharibu muungano wa Sahel kwa msaada wa Ufaransa.
Kauli hii inakuja, wakati ECOWAS ikisema inapanga keundelea na juhudi za maridhiano ya kidiplomasia yakiongozwa na marais wa Togo na Senegal, kujaribu kuwashawishi wakuu wa nchi hizo kubadilisha mawazo
Syria: Askofu alitoweka wakati wa vita alikuwa akishikiliwa na utawala
Shirika lisilo la kiserikali la Hostage Aid Worldwide limetangaza siku ya Jumanne Desemba 24, 2024 mjini Damascus kwamba askofu, raia wa Syria mwenye asili ya Marekani, Yohanna Ibrahim, aliyetekwa nyara mwaka 2013 wakati wa vita nchini Syria, alionekana katika jela chini ya mamlaka ya Bashar Al Assad miaka mitano baadaye.

“Yohanna Ibrahim ni raia wa Marekani. Alionekana mwaka wa 2018 idara ya 291, gereza la Damascus, amesema Nizar Zakka, kiongozi wa shirika hilo.
Mkuu wa Dayosisi ya Othodoksi ya Aleppo huko syria (kaskazini) alitekwa nyara pamoja na Boulos Yazigi, mkuu wa dayosisi ya Othodoksi ya Ugiriki ya jiji hilo, mwezi wa Aprili 2013 karibu na Aleppo. Utawala wa Syria ulinyooshea kidole cha lawama “wanajihadi wa Chechnya” kwa kumteka nyara kiongozi huyo wa kidini.
Wakati huo huo shirika lisilo la kiserikali la Hostage Aid Worldwide limetangaza Jumanne hii mjini Damascus kwamba liko na “data” ambazo zinonyesha kwamba mwandishi wa Marekani Austin Tice, aliyetoweka nchini Syria tangu 2012, ” yuko hai”. “Tuna data kwamba Austin alikuwa hai hadi Januari 2024, na Rais wa Marekani alisema mnamo Agosti kwamba yu hai, na tuna imani kuwa yuko hai leo,” amesema Nizar Zakka, rais wa shirika hili ambalo linafanya kazi na familia ili kuwaachilia raia waliotekwa nyara.
Brazil yasitisha ujenzi wa kiwanda cha BYD kutokana na ‘’hali ya utumwa’’ kwa wafanyakazi
Mamlaka ya Brazil imezuia ujenzi wa kiwanda cha magari ya umeme cha kampuni ya China, BYD, baada ya kugundua kwamba wafanyakazi walikuwa wakifanya kazi katika mazingira ya “utumwa.”
Zaidi ya wafanyakazi 160 walinusuriwa kutoka jimboni Bahia, ambapo walikuwa wakiishi katika hali mbaya, wakifungwa pasi za kusafiri na mishahara yao kushikiliwa na kampuni ya ujenzi ya Jinjiang Construction Brazil.
Wafanyakazi walikuwa wanalazimika kulala kwenye vitanda bila magodoro, na matumizi ya vyoo yalishirikishwa na wafanyakazi 31. Hali ya malazi ilionyesha picha ya uchache na unyanyasaji, na kuonekana kama “hali ya utumwa” kwa mujibu wa sheria za Brazil. Wafanyakazi wengi walikumbwa na kazi ya kulazimishwa na waliachwa bila malipo.
BYD ilisema kuwa imevunja uhusiano na kampuni hiyo na itaendelea kuzingatia sheria za Brazil. Kampuni hiyo imehamisha wafanyakazi kwenye hoteli na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu hali ya kazi na malazi ya wafanyakazi wake.
BYD, kampuni kubwa ya kutengeneza magari ya umeme, ililenga kuwa na kiwanda chake cha kwanza cha magari ya umeme nje ya Asia ifikapo Machi 2025.
Mwaka 2023, BYD iliuza magari mengi zaidi ya umeme kuliko Tesla , na hivyo kujiweka katika ushindani mkubwa na kampuni ya Elon Musk katika sekta hii.
Lakini kuna ongezeko la upinzani nje ya nchi dhidi ya kile ambacho wengine wanaona kama serikali ya China haiwapigi jeki watengenezaji magari nchini humo.
Masoko makubwa kama vile Marekani na Ulaya yameweka ushuru kwa magari ya umeme kutoka China, huku ushuru zaidi ukitarajiwa wakati wa utawala unaokuja wa rais mteule wa Marekani Donald Trump.
American Airlines inasema safari za ndege zimeanza tena baada ya huduma zote kusitishwa

Inaonekana hitilafu ya kiufundi ya Shirika la Ndege la Marekani imetatuliwa, huku abiria wakisema wameanza kuabiri ndege.
Kufikia sasa Shirika la safari za Anga halionyeshi kuwa kuna ucheleweshaji mkubwa katika viwanja vya ndege vya Marekani, lakini tutasubiri kuona jinsi hilo litakavyokuwa.
Sasa ‘hali imerejea kama kawaida’ – abiria wa Chicago
Sasisho kwenye mitandao ya kijamii, kutoka kwa mwanzilishi wa tovuti ya usafiri wa anga AirlineGeeks.com, Ryan Ewing umeonyesha hali imerejea kama kawaida.
Ujumbe kwenye mtandao wa X, unasema kumekuwa na tangazo, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chicago O’Hare, kuwa mfumo sasa “uko sawa”.
Anaongeza kuwa afisa “ameelekeza abiria kwenda langoni”.
Shirika la ndege la Marekani limesimamisha safari zote za ndege
Ni mwanzo wa siku ya usafiri yenye shughuli nyingi za Mkesha wa Krismasi nchini Marekani na Shirika la ndege za Marekani limesitisha safari zake zote.
Hili limetokana na tatizo la kiufundi, kulingana na shirika hilo la ndege, ambalo wanasema wanajaribu kulitatua haraka iwezekanavyo.
Agizo la kusitisha safari za ndege ni kwa viwanja vya ndege vyote, kulingana na ujumbe.
Meli ya Urusi yazama baada ya kutokea kwa mlipuko katika chumba cha injini

Meli ya mizigo ya Urusi, Ursa Major, imezama katika bahari ya Mediterania kati ya Uhispania na Algeria baada ya kutokea kwa mlipuko katika chumba cha injini, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imethibitisha.
Ilisema wanachama 14 wa wafanyakazi waliokolewa na kupelekwa katika bandari ya Uhispania ya Cartagena lakini wengine wawili hawakupatikana.
Ursa Major aliondoka bandarini huko St Petersburg siku 12 zilizopita, kulingana na shirika la habari la Urusi Interfax.
Mmiliki wa meli hiyo alisema ilikuwa ikielekea Vladivostok Mashariki ya Mbali nchini Urusi ikiwa imebeba korongo mbili za bandari zenye uzito wa tani 380 kila moja, ingawa haikuweza kuthibitishwa kwa kujitegemea.
Ursa Major alikuwa katika eneo moja la Med na meli nyingine ya Urusi iliyoidhinishwa, Sparta, ilipokumbwa na matatizo na meli hizo mbili zilionekana zikipitia kivuko cha Uingereza wiki iliyopita.
Mapema mwezi huu, idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine iliripoti kwamba Sparta ilikuwa ikielekea katika kambi ya jeshi la wanamaji la Urusi kwenye pwani ya Syria huko Tartous kuhamisha zana za kijeshi kutoka Syria baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.
Maandamano yaibuka Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi

Maandamano yameibuka nchini Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi karibu na jiji la Hama.
Video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha wapiganaji waliovaa barakoa wakichoma mti ulioonyeshwa kwenye uwanja mkuu wa Suqaylabiyah, mji unaoongozwa na Wakristo katikati ya Syria.
Kundi kuu la Kiislamu linaloongoza mapinduzi yaliyomuondoa Rais Bashar al-Assad limesema kwamba watu waliotekeleza tukio la kuchoma mti ni wapiganaji wa kigeni na tayari wametiwa nguvuni.
Maelfu ya waandamanaji walijitokeza mitaani kote nchini, wakiitaka serikali mpya ya Kiislamu kulinda haki za wachache wa kidini.
Picha za tukio hilo zilionyesha kiongozi wa kidini kutoka kwa kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) akiwahakikishia watu waliojitokeza Suqaylabiyah kuwa mti huo utarekebishwa kabla ya asubuhi. Kiongozi huyo alionyesha msalaba kama ishara ya mshikamano, jambo ambalo wahafidhina wa Kiislamu wangeepuka kufanya.
Katika eneo la Bab Touma la Damascus, waandamanaji walibeba msalaba na bendera za Syria, wakisema “Tutatoa roho zetu kwa ajili ya msalaba wetu”.
“Mambo ikiwa hayaturuhusu kuishi imani yetu ya Kikristo nchini mwetu, kama tulivyokuwa tukiishi zamani, basi hatustahili kuwa hapa tena,” alisema mtetezi mmoja aitwaye Georges kwa shirika la habari la AFP.
Syria ina makundi mengi ya kikabila na kidini, ikiwa ni pamoja na Wakurdi, Waarmenia, Waashuru, Wakristo, Druz, Waislamu wa Kishia wa Alawite na Waislamu wa Sunni, ambao ni wengi kati ya Waislamu.
Viongozi wa HTS walizungumza kuhusu kujenga Syria kwa ajili ya Wasyiria wote, na kusema kwamba haki na uhuru wa wachache wa kidini na kikabila watalindwa.
Ijumaa, Marekani iliondoa dau la $10 milioni kwa mkuu wa HTS, Ahmed al-Sharaa, baada ya mazungumzo kati ya mabalozi wa juu na wawakilishi wa kundi hilo.
Marekani inaendelea na uwepo wake wa kijeshi Syria. Imetangaza Ijumaa kwamba ilifanya shambulio la angani katika mji wa kaskazini wa Deir Ezzor, na kuua wanachama wawili wa kundi la jihadi la Islamic State (IS).
Uwepo wa wapiganaji wa kigeni, wanaharakati wa Kiislamu, au hata wafuasi wa utawala ambao wanavutiwa na kuleta usalama na kushambulia wachache ni changamoto kubwa ambayo uongozi mpya wa Kiislamu utakuwa nayo.
Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alazwa hospitalini

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amelazwa hospitalini baada ya kupata homa, kwa mujibu wa msemaji wa chama cha Democrat.
“Anasalia katika hali nzuri na anathamini sana utunzaji bora anaopokea,” Angel Ureña aliandika kwenye X, iliyokuwa Twitter.
Alisema Clinton alilazwa katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Georgetown huko Washington, DC siku ya Jumatatu jioni kwa ajili ya vipimo na uchunguzi baada ya kupata homa hiyo.
Taarifa ya Bw Ureña haikutoa maelezo zaidi kuhusu hali ya mwanachama huyo wa demokrat kutoka Arkansas, ingawa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha Clinton anatarajiwa kupata nafuu.
Chombo cha anga za mbali chajaribu kulikaribia jua

Chombo cha anga za juu cha NASA kinajaribu kuweka historia kwa kuwa karibu zaidi na jua.
Chombo hicho cha Parker Solar Probe kilisafiri katika angahewa ya nje ya nyota yetu, kikistahimili joto na mionzi mikali.
Hakitakuwa na mawasiliano yoyote kwa siku kadhaa wakati huu wa joto kali na wanasayansi watakuwa wakisubiri ishara, inayotarajiwa tarehe 27 Desemba, kuona ikiwa kimenusurika.
lengo ni kwamba uchunguzi unaweza kutusaidia kuelewa vyema jinsi Jua linavyofanya kazi.
Dkt Nicola Fox, mkuu wa sayansi katika Nasa, aliiambia BBC News: “Kwa karne nyingi, watu wamejifunza kuhusu Jua, lakini hupati uzoefu wa mazingira ya mahali hadi utakapotembelea.
“Na kwa hivyo hatuwezi kuona anga ya nyota yetu isipokuwa iwapo tutaipitia.”
Chombo hicho cha Parker Solar Probe kilizinduliwa mwaka wa 2018, kuelekea katikati mwa Mfumo wetu wa Jua.
Tayari kimepita karibu na Jua mara 21, ikikaribia zaidi, lakini ziara ya Mkesha wa Krismasi ni ya kuvunja rekodi.
Kwa kukaribia kwake, chombo hicho kiko umbali wa maili milioni 3.8 (kilomita milioni 6.2) kutoka kwenye uso wa jua
Hii inaweza isionekane kuwa karibu, lakini Nicola Fox wa Nasa anaelezea katika mtazamo wake: “Tuko maili milioni 93 kutoka kwa Jua, kwa hivyo nikiweka Jua na Dunia umbali wa mita moja, Parker Solar Probe iko sentimita nne kutoka kwa Jua – kwa hivyo hiyo ni karibu.”
Uchunguzi utalazimika kustahimili halijoto ya 1,400C na mionzi ambayo inaweza kuharibu nyaya za ndani za chombo hicho.
Mke wa mwanasiasa wa Uganda anayezuiliwa Kizza Besigye alaani marufuku ya kumtembelea siku ya Krismasi

Mke wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda anayezuiliwa Kizza Besigye ameshutumu kuwa ni “ukatili na unyama” wa kupiga marufuku wafungwa kupokea wageni siku ya Krismasi.
Besigye, 68, ameshtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa kupatikana na bastola na kujaribu kununua silaha nje ya nchi, jambo ambalo amekanusha. Kesi yake imeahirishwa hadi mwezi ujao.
Mamlaka ya magereza inasema kama sehemu ya hatua za kuzuia “kutokuwepo kwa usalama”, wafungwa hawataruhusiwa kutembelewa na wageni kwa siku saba, kuanzia mkesha wa Krismasi.
Mkewe Besigye, Winnie Byanyima, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi, alisema anapanga kupiga kambi nje ya Gereza la Luzira ili aweze kumuona mumewe na kumpa chakula siku ya Krismasi.
Mkewe Besigye, Winnie Byanyima, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi, alisema anapanga kupiga kambi nje ya Gereza la Luzira ili aweze kumuona mumewe na kumpa chakula siku ya Krismasi.
Aliiambia BBC kwamba mume wake bado ni “mwenye nguvu na mvumilivu” katika “chumba kidogo ” nyuma ya milango sita ya gereza, lakini alikuwa na wasiwasi kwamba anaweza “kudhurika”.
“Siachi chakula cha Besigye langoni [kama nilivyoelekezwa]. Nitaenda huko na kumuona mume wangu kwa sababu siwaamini hata siku moja,” Bi Byanyima alisema.
“Labda nitachukua hema na kulala huko … ikiwa ndivyo wanataka,” aliongeza.
Besigye amegombea na kushindwa katika chaguzi nne za urais dhidi ya Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.
Lakini mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani amekuwa hajishughulishi sana na siasa katika miaka ya hivi karibuni, na hakugombea uchaguzi wa 2021.
Besigye, hata hivyo, alirejea kwenye vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya kutekwa nyara vibaya akiwa ziarani Kenya na kupelekwa Uganda kwa nguvu.
Kisha alishtakiwa pamoja na msaidizi, wake Obeid Lutale. Yeye, pia, amekanusha mashtaka.
Urusi yakanusha ripoti kwamba mke wa Assad anataka talaka

Mke mzaliwa wa Uingereza wa rais aliyeondolewa madarakani wa Syria Bashar al-Assad hajaomba talaka, msemaji wa Kremlin amesema.
Ripoti katika vyombo vya habari vya Uturuki zilidokeza kuwa Asma al-Assad alitaka kuvunja ndoa yake na kuondoka Urusi, ambapo yeye na mumewe walipewa hifadhi baada ya muungano wa waasi kuupindua utawala wa rais huyo wa zamani na kuchukua udhibiti wa Damascus.
Alipoulizwa kuhusu ripoti hizo katika simu ya mkutano wa waandishi wa habari, Dmitry Peskov alisema, “Hapana, haziendani na ukweli.”
Pia alikanusha ripoti kwamba Assad alikuwa amezuiliwa Moscow na kwamba mali yake ilikuwa imehifadhiwa.
Urusi ilikuwa mshirika mkubwa wa utawala wa Assad na ilitoa msaada wa kijeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lakini ripoti katika vyombo vya habari vya Uturuki siku ya Jumapili zilidokeza kwamba Assad na mkewe walikuwa wakiishi chini ya vikwazo vikali katika mji mkuu wa Urusi, na kwamba bi Assad aliwasilisha ombi la talaka ili arudi London.
Bi Assad ana uraia wa Syria na Uingereza, lakini waziri wa mambo ya nje wa Uingereza hapo awali alisema hataruhusiwa kurejea Uingereza.
Akiongea bungeni mapema mwezi huu, David Lammy alisema: “Nataka ithibitishwe kuwa yeye ni mtu aliyewekewa vikwazo na hatakiwi hapa Uingereza.”
Aliongeza kuwa atafanya “kila niwezalo kwa uwezo wangu” kuhakikisha hakuna mwanafamilia wa Assad “anayepata nafasi nchini Uingereza”.
Katika taarifa iliyohusishwa na Bashar al-Assad wiki iliyopita, alisema hakuwahi kuwa na nia ya kutoroka Syria, lakini alisafirishwa kwa ndege kutoka kituo cha kijeshi cha Urusi kwa ombi la Moscow.
Israel yathibitisha kumuua kiongozi wa Hamas Haniyeh mjini Tehran

Waziri wa ulinzi wa Israel kwa mara ya kwanza amekiri kuwa Israel ilimuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai.
Israel Katz alitoa maoni hayo katika hotuba yake akiahidi kuwalenga wakuu wa vuguvugu la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, ambalo limekuwa likirusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel.
Haniyeh aliuawa katika jengo alimokuwa akiishi katika mji mkuu wa Iran katika shambulizi linalohusishwa na Israel.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema baadhi ya hatua zimepigwa katika kukubaliana kusitisha mapigano huko Gaza na Hamas, lakini hakuweza kutoa ratiba ya lini makubaliano yataafikiwa.
Haya yanajiri baada ya afisa mkuu wa Palestina kuiambia BBC kwamba mazungumzo kati ya Hamas na Israel yamekamilika kwa asilimia 90, lakini masuala muhimu yalisalia.
Katika hotuba yake, Katz alisema Israel “itatekeleza mashambulizi makali dhidi ya Houthis na “kukata kichwa” uongozi wake.
“Kama tulivyofanya kwa Haniyeh, [Yahya] Sinwar, na [Hassan] Nasrallah huko Tehran, Gaza, na Lebanon, tutafanya hivyo huko Hodeida na Sanaa,” alisema, akimaanisha viongozi wa Hezbollah na Hamas ambao wote wameuawa. mwaka huu.
Haniyeh, mwenye umri wa miaka 62, alizingatiwa pakubwa kuwa kiongozi wa jumla wa Hamas na alichukua jukumu muhimu katika mazungumzo yenye lengo la kufikia usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.
Baada ya mauaji yake, Hamas ilimtaja Yahya Sinwar, kiongozi wake huko Gaza na mmoja wa wasanifu wakuu wa mashambulizi ya Oktoba 7, kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo.
Sinwar aliuawa na jeshi la Israel katika pambano la kubahatisha huko Gaza mwezi Oktoba na kundi hilo bado liko katika harakati za kumchagua kiongozi mpya.
Hassan Nasrallah wakati huo huo aliyekuwa kiongozi wa kundi la Lebanon linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah – aliuawa mjini Beirut mwezi Septemba wakati Israel ikizidisha kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Hezbollah, ambayo ilikuwa ikiishambulia kila siku kwa kuvuka mpaka siku moja baada ya shambulio la tarehe 7 Oktoba.
Waasi wa Houthi, kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran ambao wanadhibiti kaskazini-magharibi mwa Yemen, walianza kushambulia meli za Israel na kimataifa katika Bahari Nyekundu muda mfupi baada ya Israel kuanza kulenga Hamas huko Gaza Oktoba iliyopita.
Kundi hilo limeapa kuendelea hadi vita huko Gaza viishe.
Je, Iran ilitengeneza vipi kombora la hypersonic ambalo linaweza kufika Israel kwa ‘sekunde 400’ licha ya vikwazo?

Katika giza la usiku wa Aprili 13, 2024, na kuba la dhahabu la Msikiti wa Al-Aqsa kwa nyuma, mwanga wa kombora la balistiki la Iran ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwenye picha ambayo pengine ulimwengu utaikumbuka kwa muda mrefu.
Shambulio hilo la kombora na ndege zisizo na rubani na Iran lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuangusha mfumo maarufu wa ulinzi wa Israel unaojulikana kama Iron Dome.
Makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani zilizorushwa kutoka Iran zilipiga maeneo mbalimbali nchini humo, ikiwemo uwanja wa ndege wa Israel.
Shambulio hilo lilirudiwa takriban miezi sita baadaye mnamo Oktoba 1, 2024.
Walinzi wa Mapinduzi ya Iran walirusha idadi kubwa ya makombora kuliko hapo awali na kulenga shabaha zaidi za Israel kuliko hapo awali.
Kulingana na William Alberc, mtafiti katika Taasisi ya Stimson na mkurugenzi wa zamani wa mpango wa udhibiti wa silaha wa NATO, shambulio la hivi karibuni la Iran limebadilisha hali ya Mashariki ya Kati milele.
Kumbuka kwamba shambulio hili liliwezeshwa na mpango wa makombora wa Iran, ambao umekuwa ukiendelea kwa kasi ya kushangaza kwa miongo kadhaa, na serikali ya Irani ina imani sana na mpango huu kwamba neno ‘pointi’ linatumika kwa makombora haya kwa sababu ya uwezo wake wa kupiga malengo.
Hivyo mpango huu wa makombora unazidi kuwa tatizo kubwa kwa ulimwengu wa Magharibi na Israel pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu katika Mashariki ya Kati.
Mpango huu wa makombora ni nini? Iran ina makombora ya aina gani na yameendelezwa kiasi gani? Je, mpango wa makombora wa Iran umekuwaje wa hali ya juu licha ya vikwazo hivi vyote? Hebu tupate majibu ya maswali haya.
Safari ya mafanikio ya mpango wa makombora wa Iran licha ya vikwazo

Kwa mujibu wa taasisi ya amani ya Marekani, Iran ina silaha kubwa zaidi na tofauti zaidi ya makombora ya balistiki katika Mashariki ya Kati. Kando na hayo, Iraq ndiyo nchi pekee katika eneo hilo ambayo haina silaha za nyuklia, lakini makombora yake ya balistiki yanaweza kushambulia hadi umbali wa kilomita 2,000.
Teknolojia ya makombora ya balistiki ilitengenezwa wakati wa Vita vya pili vya dunia , lakini ni nchi chache sana ulimwenguni ambazo zina uwezo wa kutengeneza makombora ya balistiki kwa kutumia teknolojia hii zenyewe.
Iran imepata teknolojia hii na kutengeneza makombora ya balistiki katika miongo miwili iliyopita licha ya vikwazo vikali vya kimataifa. Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei alisema katika hotuba yake ya hivi karibuni kwamba mipango ya kijeshi na makombora ambayo yalizivuruga nchi za Magharibi yote yalitengenezwa wakati wa vikwazo hivyo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio mwaka 2006. Chini ya azimio hilo, Iran ilipigwa marufuku kuuza silaha za nyuklia au nyenzo zake. Pia ilijumuisha bidhaa ambazo zingeweza kutumika kwa madhumuni mengine yoyote na kwa madhumuni ya kijeshi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio jingine miezi mitatu baadaye na pia kuweka vikwazo vya mikataba ya kawaida ya silaha na Iran. Pia inajumuisha teknolojia ya kijeshi. Pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran, mpango wa makombora ya balistiki pia ulikuja chini ya wigo wa vikwazo vilivyowekwa chini ya pendekezo hilo.
Hivyo haikuwa rahisi kwa Iran kununua silaha kutoka nchi kama vile Urusi na China. Wakati wa vita vya Iraq, Iran ilikuwa ikinunua bidhaa kutoka nchi zote mbili.
Makombora ya balistiki yana uwezo wa kutoa silaha za nyuklia, na kwa mujibu wa nchi za Magharibi, Iran inapopata teknolojia ya makombora ya balistiki, itafanya kila juhudi kupata nishati ya nyuklia na kurutubisha uranium inayohitajika kutengeneza silaha za nyuklia.

Kufuatia kukamilika kwa makubaliano ya mpango kamili wa utekelezaji kati ya Iran na madola sita makubwa duniani mwezi Julai 2015 na kuidhinishwa kwa ‘Pendekezo 2231’, vikwazo vyote vya Baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya Iran viliondolewa.
Hata hivyo, vikwazo vya silaha viliendelezwa na kifungu kinachojulikana kama “njia ya kufyatua risasi”. Chini ya mpango huo, mpango wa makombora wa Iran ulipaswa kufuatiliwa kwa karibu kwa miaka mitano. Ilikuwa ni njia ya kuweka shinikizo kwa Iran na kuzuia mpango wake wa makombora.
Kwa hakika Iran imeendeleza mpango wake wa makombora kiasi kwamba mwezi Machi 2016, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa barua ya pamoja ikiishutumu Iran kwa majaribio ya makombora na kusema kuwa Iran imekiuka sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Azimio nambari 2231” baada ya makubaliano ya JCPOA ” limekiukwa.
Hatimaye, mwaka 2020, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliamua kujiondoa kwenye makubaliano hayo. Moja ya sababu zilizoifanya Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo ni kwa sababu ya tishio la mpango wa makombora wa Iran na kukosekana kwa utaratibu unaofaa wa kufanya majaribio ya mpango huo.
Ijapokuwa Iran imejaribu kuonyesha kuwa ni sehemu ya mpango wa utekelezaji wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Iran imetangaza kuwa itanunua silaha kutoka Urusi na China mnamo Oktoba 2021, huku muda wa mwisho wa azimio nambari 2231 ukikamilika. Kwa vile vikwazo bado vipo, matakwa ya Iran hayakuweza kutimizwa.
Tangu wakati huo Iran imetengeneza zaidi ya aina 50 za roketi, makombora ya balistiki na cruise, pamoja na ndege zisizo na rubani za kijeshi, ambazo baadhi yake zimetumika katika mizozo ya kimataifa kama vile vita kati ya Urusi na Ukraine.

Wakati wa Vita vya Iraq na Iran, silaha za kivita za Iran zilikuwa na umbali wa kilomita 35, wakati jeshi la Iraq lilikuwa na makombora ya balistiki ya Scud B yenye umbali wa kilomita 300, yakilenga miji kadhaa ndani ya Iran.
Huku jeshi la Iraq likipata nguvu katika mashambulizi ya makombora, Iran nayo ilifikiria kutumia makombora, na kiongozi mkuu wa Iran wakati huo, Ruhullah Khomeini, aliiruhusu Iran kukabiliana na mashambulizi hayo ya makombora.
Shambulio la kwanza la kombora dhidi ya Irani na Iraq lilikuwa mnamo Machi 21, 1985. Ililenga mji wa Kirkuk. Siku mbili baadaye shambulio lingine la Iran lilifanyika kwenye Klabu ya Maafisa wa Jeshi la Iraq huko Baghdad, na kuua makamanda 200 wa Iraqi.
Nchi za Kiarabu na Libya ziliandamana baada ya shambulio hili la kombora la Iran. Washauri wa Libya kisha waliondoka Iran na kuzima mfumo wa makombora na kurusha kabla ya kuondoka.
Katika hali hiyo, kundi la wanachama wa Jeshi la Anga la Iran lilianza jaribio la kombora lenyewe. Kikundi kidogo cha RIGC kilianza uhandisi wake wa nyuma kwa kufungua vipuri vidogo vya roketi na vifyatuzi

Hassan Tehrani Muqaddam anaitwa baba wa mpango wa makombora wa Iran. Katika makala iitwayo ‘Programu ya Kombora Zero kwa Mia Moja’, Hassan Tehrani anasema kwamba wanachama 13 wa Walinzi wa Mapinduzi walipelekwa Syria kwa mafunzo ya makombora ya balestiki ya Scud baada ya washauri wa Libya kuondoka Iran. Alielewa kazi ya kombora la Scud ndani ya muda mdogo.
Muqadam aliteuliwa kuwa Kamanda wa Makombora wa Jeshi la anga la Iran mnamo 1986. Kisha mnamo 1988, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Irani kilianza juhudi kubwa za kuunda makombora.
Katika miaka ya 1990, Korea Kaskazini na kisha China pia walijitokeza kusaidia Iraq na mpango wake wa makombora. Kwa sababu hiyo, majaribio ya baadhi ya mataifa makubwa duniani kutaka China kuwa sehemu ya ‘utawala wa kudhibiti teknolojia ya makombora’ hayajafanikiwa.
Udhibiti wa Teknolojia ya Makombora ni makubaliano ya kisiasa yasiyo rasmi kati ya nchi 35 wanachama ili kupunguza uzalishaji, ukuzaji na teknolojia ya makombora. China haikukubali kuwa mshiriki wake, lakini ilihitaji kujitolea kufuata masharti ya makubaliano hayo.
Roketi za ‘Naejat’ na ‘Mujtama’ zilikuwa roketi za kizazi cha kwanza kutengenezwa nchini Iran. Mara tu baada ya hapo, kombora la ‘Thunder 69’ lilitengenezwa. Kwa kweli ni kombora la masafa mafupi la Uchina B610, iliyoundwa upya kwa vikosi vya jeshi la Irani.
Awamu ya pili na mbaya zaidi ya mpango wa makombora wa Iran ilianza kwa utengenezaji wa kombora la Fatah 110.
Kwa mujibu wa Iran, Hassan Muqaddam alikuwa akijiandaa kwa jaribio jipya la kombora wakati milipuko miwili ilipotokea na kuuawa katika mlipuko wa pili. Sababu halisi ya mlipuko huo haikujulikana kamwe, lakini jiwe la kaburi la Hassan Muqadam lilisemekana kumzika mtu ambaye alitaka kuiangamiza Israel.
Hivi sasa, Kikosi cha wanaanga cha walinzi wa mapinduzi, kinachoongozwa na Amir Ali Hajazada, ndicho chombo kikubwa zaidi cha kutengeneza makombora na ndege zisizo na rubani kwa vikosi vya jeshi la Iran. Kwa kweli, kwa miaka kadhaa iliyopita, shirika hili limefanya kazi kwa Irani nje ya nchi badala ya jeshi la Irani.
Mji wa makombora ulio chini ya ardhi

Vyombo vya habari vya Iran na walinzi wa mapinduzi wametoa picha kadhaa za maghala ya makombora ya chinichini kufikia sasa.
Iran inaendelea kuonyesha kombora na silaha zake za kijeshi kama mafanikio makubwa, lakini mpango wake wa makombora na maendeleo ya maghala ya makombora ni siri.
Kamanda wa jeshi la anga la IRGC Amir Ali Hajizada alizungumza kwa mara ya kwanza mwaka 2014 kuhusu vituo hivyo vya kuhifadhia makombora vilivyojengwa mita 500 chini ya ardhi katika mikoa mbalimbali ya Iran.
Hakuna habari ya kuaminika inayopatikana kuhusu wakati maghala haya ya chini ya ardhi yalijengwa. Katika mahojiano na gazeti la Al Jazeera, Mehdi Bakhtiari, mwandishi wa idara ya kijeshi ya shirika la habari la Iran amesema kuwa, ghala la kwanza la kuhifadhia makombora ya chini ya ardhi magharibi mwa Iran lilijengwa mwaka 1984, na hapo ndipo mpango wa makombora wa Iran ulipoanza.
Picha ya moja ya ghala hizo za siri za chini ya ardhi inaaminika kuwa ghala la pili kwa ukubwa. Inahifadhi silaha muhimu zaidi za kombora na droni za Walinzi wa mapinduzi.
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kilitangaza mnamo Machi 2019 ‘mji wa kombora la bahari’ kwenye mwambao wa Ghuba ya Uajemi. Mahali halisi ya kituo hicho hakikufichuliwa kama hapo awali, lakini vyombo vya habari vya ndani katika mkoa wa Harmuzkan viliripoti kuhusu msingi huo.
Kamanda Mkuu wa Walinzi wa mapinduzi wa Iran, Hossein Salami, alipokuwa akizungumzia ‘Mji wa Kombora wa Marion’ katika mwambao wa Ghuba ya Uajemi, alisema kuwa kiwanja hiki ni moja ya vituo vya jeshi la majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, ambapo makombora ya kistratejia yanahifadhiwa.
Hakuna anayejua idadi kamili ya maghala kama hayo ya chini ya ardhi ya makombora ambayo Iran inayo, lakini kamanda wa jeshi la Iran Ahmad Raza Pordistan alitangaza Januari 2014 kwamba mji wa chini ya ardhi wa makombora haukuwa wa Walinzi wa Mapinduzi pekee.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.