Sudan Kusini ‘imezidiwa’ na idadi kubwa ya wakimbizi na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Sudan Kusini inazidiwa uwezo kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi wanaokimbia vita nchini Sudan pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, hii ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka RSF.

Wanawake waliokimbia Sudan iliyokumbwa na vita kufuatia kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye foleni ya kupokea mgao wa chakula katika kituo cha usafirishaji cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
Wanawake waliokimbia Sudan iliyokumbwa na vita kufuatia kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye foleni ya kupokea mgao wa chakula katika kituo cha usafirishaji cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) REUTERS – JOK SOLOMUN

Kwenye taarifa yake, shirika hilo limesema watu karibu elfu 5 wanavuka mpaka wa nchi hizo mbili kila siku, takwimu zinazouwiana na zile za umoja wa Mataifa zinazoonesha ni watu kati ya elfu 7 na elfu 10 wanavuka mpaka kila siku.

Sudan inakabiliwa na moja ya mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani uliochochewa na vita kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa RSF tangu mwezi April mwaka uliopita, ambapo umesababisha maelfu ya watu kuuawa na mamilioni kuwa wakimbizi.

Wakimbizi wa Sudan wamekusanyika katika kambi ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini Sudan.
Wakimbizi wa Sudan wamekusanyika katika kambi ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) nchini Sudan. VIA REUTERS – Mohammad Ghannam/MSF

Ofisi ya MSF nchini Sudan imetolea mfano kambi ya wakimbizi ya Renk inayohifadhi raia zaidi ya elfu 17, kuwa imezidiwa uwezo na huenda hali ikawa mbaya zaidi ikiwa msaada wa dharura hautatolewa kwa wakati.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment