Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Tangu mwishoni mwa juma lililopita kumeendelea kuripotiwa mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali wanaosaidiwa na wapiganaji Wazalendo dhidi ya waasi wa M23 wanaosaidiwa na nchi ya Rwanda.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mapigano yaliripotiwa kwenye eneo la Lubero lililoko umbali wa kilometa 150 kaskazini mwa mji wa Goma.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha mwaka mmoja, jeshi lilitumia helikopta za kivita kuwakabili waasi wa M23, ikiwa ni katika juhudi za kuzidisha udhibiti wao hadi mji wa Alimbongo baada ya kufanikiwa kuteka eneo la Mambasa na Kanyabi.

Makabiliano yameongezeka zaidi tangu kutangazwa kuvunjika kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yanaratibiwa na Serikali ya Angola.
Mashirika ya kiraia wilayani Lubero yanasema mapigano haya yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wanaokimbia makazi yao.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.