WHO: Ugonjwa wa Mpox barani Afrika bado ni dondasugu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la afya duniani WHO, linasema mwenendo wa maambukizo ya virusi vya Mpox barani Afrika bado ni hatari, huku nchi za DRC, Burundi na Uganda zikiendelea kurekodi wagonjwa zaidi.

Mgonjwa mwenye ugonjwa wa kupooza akipatiwa matibabu katika jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwezi Agosti. Mlipuko wa ugonjwa nchini DRC ambao umeenea hadi nchi jirani umeliweka Shirika la Afya Duniani katika hali ya tahadhari, na kutangaza dharura ya afya ya umma duniani.
Mgonjwa mwenye ugonjwa wa kupooza akipatiwa matibabu katika jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwezi Agosti. Mlipuko wa ugonjwa nchini DRC ambao umeenea hadi nchi jirani umeliweka Shirika la Afya Duniani katika hali ya tahadhari, na kutangaza dharura ya afya ya umma duniani. © Arlette Bashizi/Reuters

Kulingana na ripoti ya WHO, bara Afrika limerekodi wagonjwa zaidi ya elfu 13 katika mataifa 20 hadi kufikia Desemba 15 mwaka huu, ikiwemo vifo, huku nchi ya DRC ikiwa ndio imeathiriwa zaidi.

Aidha licha ya maambukizo nchini DRC kuonekana kudhibitiwa katika majuma ya hivi karibuni, WHO bado inaonya kuwa mamlaka hazipaswi kubweteka badala yake tahadhari zaidi zinafaa kuchukuliwa.

Wataalamu wa afya wamekuwa na hofu ya kuenea zaidi kwa virusi hivyo kutokana na aina mpya ya kirusi kilichopewa jina la 1b, ambacho pia kimeripotiwa kwenye nchi za Sweden na Thailand.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment