DRC: Takriban watu 40 wakufa maji baada ya boti kuzama katika mkoa wa Équateur

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

DRC inaendelea kukumbwa na ajali za majini na kusababisha vifo vya watu wengi. Ajali nyingine ilitokea kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku ya Alhamisi Desemba 19, 2024. Boti iliyokuwa ikitokea katika bandari ya Lolo, katika eneo la Inende, ilizama baada ya kupakia kupita kiasi. Iliondoka bandarini kuelekea Mbandaka; idadi ya awali ni watu 40 ambao wamefariki na karibu mia kadhaa hawajulikani waliko.

Muonekano wa jumla wa boti iliyotengenezwa kwa mbao kwenye Mto Kongo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 31, 2024.
Muonekano wa jumla wa boti iliyotengenezwa kwa mbao kwenye Mto Kongo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 31, 2024. AFP – ARSENE MPIANA

Joseph Bayoko Lokondo, mwanaharakati wa mashirika ya kiraia katika mkoa wa Équateur, kaskazini-magharibi mwa DRC, anaelezea kile kilichotokea: “Boti hiyo iliyojulikana kwa jina la Mama Witi ilikuwa imepakia kupita kiasi. Kuna watu hawajulikani waliko na zoezi la kuwatafuta linaendelea. Ajali hii ilitokea zaidi ya kilomita 160 kutoka mji mkuu wa mkoa, Mbandaka kwenye Mto Lolonga, kijito cha Mto Kongo.

Joseph Bayoko Lokondo anahakikisha kwamba walionusurika wameachwa bila msaada: “Mpaka itakapothibitishwa vinginevyo, hakuna mamlaka yoyote, hata ya mtaa au ya mkoa, iliyochukua hatua ya kuchukuwa miili hiyo. Ninawasiliana na walionusurika leo ambao wanalala nje huko Lolo. Miili iliyopatikana ilizikwa na raia waliojitolea. Hakuna timu ya uokoaji, ni wanakijiji ambao wamejipanga kujaribu kuendelea kutafuta maiti. “

“Sababu zile zile ndizo husababisha ajali”

Kwa mujibu wa Joseph Bayoko Lokondo, ni mzigo kupita kiasi, lakini juu ya yote kutokuwepo kwa koti la kujiokoa ambalo husababisha ajali kama hizo ingawa hatua zilikuwa zimetangazwa. “Ni sababu zile zile ambazo usababisha ajali, ni mzigo kupita kiasi, ni safari za usiku. Naye Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri wa Uchukuzi walitoa agizo la kuwataka wasafiri wote wa mtoni waweze kupata koti za kujiokoa. Lakini uamuzi huu unaonekana kupuuzwa na mamlaka ya utawala wa kisiasa ya mkoa wa Équateur, ambao huwaacha watu kusafiri bila koti za kujiokoa. »

“Mamlaka za kisiasa lazima zishirikiane na kamishna wa mto. Ni yeye anayeangalia usafiri majini. Wamiliki wengi wa boti wamefahamiana na kamishna wa mto na wengine wanatoa pesa kuwaruhusu abiria kusafiri hivyo, wakisema kuwa koti za kuokoa maisha zitakuwa ghali, anabainisha mwanaharakati huyo wa mashirika ya kiraia. Mamlaka lazima zione njia za kufanya mambo kuwalinda raia wenzao. “

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment