Ethiopia: Emmanuel Macron ajadili masuala ya kikanda na kutoa wito wa ‘kuweka silaha chini’ Sudan.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baada ya Djibouti, ambako alikwenda kukutana na jeshi la Ufaransa na ambako alipokelewa siku ya Jumamosi asubuhi, Desemba 21, na Rais Ismaïl Omar Guelleh, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekwenda Ethiopia kwa mkutano na rais wa nchi hiyo Abiy Ahmed. 

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, mjini Addis Ababa, Desemba 21, 2024.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, mjini Addis Ababa, Desemba 21, 2024. AFP – LUDOVIC MARIN

Kufuatia mazungumzo na Waziri Mkuu wa EthiopiaEmmanuel Macron ametoa wito kwa wapiganaji nchini Sudani “kuweka chini silaha zao” baada ya mwaka mmoja na nusu wa vita ambavyo vimeharibu nchi hiyo, akibaini kwamba njia pekee inayowezekana ni “kusitisha mapigano” na kuanzisha mazungumzo”.

Kando ya njia inayounganisha uwanja wa ndege katikati mwa mji mkuu wa Ethiopia, Picha ya Emmanuel Macron na bendera ya Ufaransa huonyeshwa kwenye mabango mengi ya matangazo. Ishara ya kwanza ya rais wa Ufaransa alipowasili ilikuwa ni kuweka shada la maua kwenye mnara wa Mapigano ya Adoua, vita vya kihistoria vilivyoashiria ushindi mkubwa wa Ethiopia dhidi ya Italia mwaka 1896.

Baada ya sherehe hizo, rais wa Ufaransa alielekea kwenye Ikulu ya Kitaifa, jengo lililojengwa mnamo mwaka 1955 kusherehekea yubile ya fedha ya utawala wa Mfalme Haile Selassie.

Kazi ya ukarabati na mabadiliko ya jengo hili kuwa jumba la makumbusho ilifadhiliwa na AFD, Shirika la Maendeleo la Ufaransa. Baada ya kutembelea makumbusho hayo, Emmanuel Macron alizungumza na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia. Mazungumzo yaliyofuatiwa na chakula cha jioni, masuala ya kuzungumzia hayakosi kwa wawili hao, kutoka kwa mwelekeo wa nchi mbili hadi makubaliano ya kumaliza mvutano kati ya Ethiopia na Somalia, pamoja na hali ya ndani nchini Ethiopia.

Upatikanaji wa Bahari Nyekundu, suala kuu kwa Ethiopia

Lengo kuu la Ethiopia, nchi isiyo na bahari katika Pembe ya Afrika, ni kwamba nchi hiyo inatafuta ufikiaji wa Bahari ya Shamu. Suala ambalo lilizua mvutano mkali na nchi jirani ya Somalia wakati mwezi Januari, Addis Ababa ilitia saini mkataba wa maelewano na jimbo lililojitenga la Somaliland kukodisha kilomita 20 za ukanda wa pwani. Mradi wa kufikia bahari ambao Waziri Mkuu wa Ethiopia jana aliomba msaada kutoka Ufaransa.

“Ethiopia ina wakazi milioni 130, uchumi unakua kwa kiasi kikubwa na kwa hili, ni nchi ambayo itahitaji upatikanaji wa bahari kwa njia ya amani, ya kidiplomasia kwa kushirikiana na nchi ndugu kama Ufaransa,” amesema Abiy Ahmed.

Emmanuel Macron amesema yuko tayari kuingilia kati suala hili nyeti sana. Rais akiuona mradi huu kuwa halali: “Alichosema Waziri Mkuu kuhusu upatikanaji wa bahari, haja ya Ethiopia kubadilisha njia yake ya kufikia, kuwa na udhibiti wa hatima yake katika mazingira ya kikanda ambayo ni magumu sana ni ombi halali. Na Ufaransa inatamani jukumu inayoweza kuchukua kwa unyenyekevu mkubwa kusaidia mchakato huu wa mseto kwa njia ya mazungumzo ya amani, yenye uwajibikaji, yenye heshima ya sheria za kimataifa na majirani zake na ni kwa roho hii kwamba tutasonga mbele na kwamba tutasaidia kuleta maendeleo yenye usawa ya Ethiopia na kanda. “

Mnamo Desemba 11, chini ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud, walikubaliana kuruhusu Ethiopia kupata njia ya baharini bila kusababisha madhara kwa Mogadishu.

Emmanuel Macron atoa wito wa “kusitishwa kwa mapigano” nchini Sudani

Rais wa Ufaransa amezungumza kuhusu hali ya Sudani na Waziri Mkuu wa Ethiopia. Akikumbusha kwamba Ufaransa iliandaa mkutano wa kimataifa mjini Paris mwezi Aprili, Emmanuel Macron alitoa wito kwa pande zinazozozana nchini Sudani kuweka chini silaha zao.

Tunatoa wito kwa wadau kuweka silaha zao chini na kwa wadau wote wa kikanda wanaoweza kutekeleza jukumu hilo, wafanye hivyo kwa njia nzuri, kwa maslahi ya watu ambao wameteseka sana. Mchakato pekee unaoweza kuwepo nchini Sudani ni ule wa kusitisha mapigano, kuanzisha mazungumzo na kurejesha nafasi yake kwa mashirika ya kiraia ambayo ilikuwa ya kupendeza sana katika mapinduzi ambayo iliweza kuongoza.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment