Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Ofisi ya takwimu ya Nigeria iko chini ya shinikizo baada ya kuchapishwa kwa uchunguzi kuhusu uhalifu na ukosefu wa usalama nchini humo. Siku chache baada ya kuchapishwa kwa utafiti huu, ambao unatoa maelezo ya kutisha ya hali ya usalama nchini, tovuti ya chombo cha serikali ilizimwa na mkuu wake ameitwa na usalama wa taifa katika hatua hiyo.

Takwimu zilizomo katika ripoti ya Ofisi ya Takwimu kuhusu “mtazamo wa uhalifu na uzoefu wa ukosefu wa usalama nchini Nigeria” ni za kutisha. Utafiti huu uliozinduliwa siku ya Jumanne unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 2 walitekwa nyara katika kipindi cha mwaka mmoja nchini humo. Lakini uaminifu wa ripoti hiyo unaonekana kutiliwa shaka hata katika ngazi za juu serikalini.
Mtakwimu mkuu anayesimamia kazi ya chombo hiki kinachohusika na kutoa data rasmi aliitwa siku ya Alhamisi jioni na DSS, Idara ya ujasusi ya ndani nchini Nigeria, chombo chenye nguvu nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya ndani, Semiu Adeyemi Adeniran aliulizwa kuhusu mbinu ya uchunguzi huu na takwimu zilizotajwa katika kurasa zake.
Utafiti huu rasmi unapendekeza kuwa Wanigeria milioni 2 walitekwa nyara kati ya mwezi Mei 2023 na Aprili 2024 na kwamba jumla ya fidia iliyolipwa ili kuwaachilia ilizidi euro bilioni 1 katika kipindi hiki.
Lakini habari hii haipatikani tena kwa umma kwa ujumla kwa kuwa tovuti ya Ofisi ya Takwimu sasa imezimwa kabisa.
Kiuhalisia, ilikuwa ni “udukuzi”, lakini Atiku Abubakar, kiongozi wa chama cha upinzani cha PDP, ameelezea tukio hili la kiufundi kama “la kutiliwa shaka”. Katika taarifa, ameonya dhidi ya jaribio lolote la kutumia takwimu rasmi kwa leno la kupotosha.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.