Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Baraza la Wawakilishi la Marekani siku ya Alhamisi Desemba 19 lilikataa kwa kiasi kikubwa muswada mpya wa bajeti ya chama cha Republican yenye lengo la kuepusha kuzorota kwa serikali ya shirikisho, hali ngumu ambayo inaongeza hali ya sintofahamu kabla ya saa mbaya ya Ijumaa usiku wa manane.

Mjini Washington, katika kumbi za Baraza la Congress, kwa mara nyingine kumetokea hali ya sintofahamu na viongozi waliochaguliwa wamegawanyika pakubwa. hali ambayo haijashuhudiwa katika historia ya Marekani, anaeleza mwanahabari wetu nchini Marekani, Loubna Anaki.
Viongozi waliochaguliwa wa chama cha Republican, licha ya kuwa na wingi wa kura katika bunge la chini, waliweka pendekezo hili jipya kwenye kura siku moja baada ya Donald Trump na Elon Musk kuvunja makubaliano ya awali yaliyojadiliwa na Wademocrats ambayo yangeepuka “kuzorota kwa shughuli za serikali” nchini Marekani kabla ya Krismasi.
Rais Mteule wa Marekani hata hivyo ametoa baraka zake kwa rasmu mpya ya Republican, akikaribisha “makubaliano mazuri sana kwa watu wa Marekani”. Kabla ya kura hiyo, kiongozi wa Wademocrats katika Baraza la Wawakilishi, Hakeem Jeffries, alielezea upinzani wake kwa pendekezo hili, “sio kubwa” na “la kicheko” kulingana na yeye. Na ingawa thuluthi mbili ya kura zilihitajika ili kupitishwa, rasimu hii haikufikia hata wingi wa kura, huku Warepublicans 38 wakijiunga na kura ya “Hapana” ya Wademocrats.
Hatua sasa haina uhakika kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Republican, Mike Johnson, alishinikiza upande mmoja na Wademocrats kurejea makubaliano yaliyojadiliwa, na kwa upande mwingine na baadhi ya maafisa wa kihafidhina waliochaguliwa ambao wanakataa kila kitu kabisa haitajumuisha kupunguzwa kwa bajeti ili kufidia msaada huo mpya.
Mazungumzo ya mwisho kabla ya “Shutdown”
Baada ya tangazo kwamba hakutakuwa na kura nyingine Alhamisi jioni, Mike Johnson ameahidi kwamba viongozi waliochaguliwa “wangekutana na kutafuta suluhisho lingine”. Muda unaisha kabla ya saa ya mbaya ya saa sita usiku Ijumaa jioni. Kupooza kwa huduma za umma za shirikisho kunaweza kusababisha ukosefu wa ajira wa kiufundi kwa mamia ya maelfu ya watumishi wa umma, kufungwa kwa manufaa kadhaa ya kijamii au hata kufungwa kwa baadhi ya vituo vya kulelea watoto mchana. Hali isiyopendeza sana, haswa Krismasi inapokaribia.
Uwezekano wa “kuzima” uliongezeka sana wakati Donald Trump alipoelezea kutoidhinisha kwake mswada siku ya Jumatano uliojadiliwa na Warepublican na Wademocrast katika Bunge la Congress, uliochukuliwa kuwa “ujinga na wa gharama kubwa” na rais mteule.
Kwa upande wa chama cha Democratic, Donald Trump na Elon Musk wanashutumiwa kwa kushindwa bajeti ya maelewano iliyopatikana kwa bidii, ingawa bado hawajatawala. “Ikiwa kutakuwa na kuzorota kwa shughuli za serikali, itakuwa kosa la Elon Musk na Donald Trump,” Hakeem Jeffries, kiongozi wa wachache wa chama cha Democratic katika Bunge hilo amesema.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.