Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini DRC kumefaanyika mabadiliko katika uongozi wa jeshi la nchi hiyo (FARDC). Rais wa DRC Félix Tshisekedi alifanya msururu wa uteuzi katika muktadha wa kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa nchi na kuendelea kusonga mbele kwa M23, haswa katika eneo la Lubero, mkoani Kivu Kaskazini. Miongoni mwa maamuzi haya, mkuu wa jeshi, FARDC, amefutwa kazi.

Jenerali Christian Tshiwewe Songesha anaacha nafasi yake kama mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa miaka miwili.
Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Walinzi wa Jamhuri, alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa majeshi mnamo Oktoba 2022 kwa dhamira ya kukabiliana na kusonga mbele kwa M23, kundi la waasi linaloungwa mkono na Rwanda.
Hata hivyo, hali ya usalama imezorota.
Hadi sasa, M23 inadhibiti maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Masisi, Rutshuru, Walikale, Nyiragongo na Lubero, maeneo ambayo kiwango chake sasa ni mara mbili ya yale yaliyokaliwa mwaka 2012.
Jenerali Tshiwewe ameteuliwa kuwa mshauri wa kijeshi wa Rais Félix Tshisekedi.
Luteni Jenerali Banza Mwilambwe Jules ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi
Mrithi wake kama mkuu wa jeshi la FARDC ni Luteni Jenerali Banza Mwilambwe Jules.
Kabla ya kupandishwa cheo, Luteni Jenerali Banza Mwilambwe Jules alishikilia nafasi ya naibu mkuu wa masuala ya kijeshi katika ofisi ya rais. Mmoja wa watu ambao rais anaamini, hapo awali aliwahi kuwa naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wa Jamhuri.
Mabadiliko mengine maarufu yanahusu uongozi wa idara ya ujasusi wa jeshi.
Meja Jenerali Christian Ndaywel, ambaye alikuwa mjuu wa idara ya ujasusi, sasa amepewa jukumu la kuongoza jeshi la nchi kavu.
Makamanda wengine wameteuliwa na wengine kubadilishiwa maeneo yao ya kazi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.