Tusipofanya Dunia Itakosa Ladha Yetu.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya sababu kubwa inayotukwamisha watu wengi kutoishi vipaji vyetu, na kutotimiza ndoto zetu ni kuacha kufanya kwa kuwa watu wengine wengi, walifanya/wanafanya kitu kinachofanana na kile unachotaka kufanya.

Ni dhahiri kuwa umewahi kuwasikia watu au pengine umekuwa ukijisimea mwenyewe kwamba, mimi naweza kufanya kitu fulani LAKINI nimeona tu niache maana watu wengi wanafanya kitu hicho. Mara nyingi utasikia mtu akijisemea, mimi ni mwandishi, mfanyabiashara, mwimbaji n.k. ila sijaamua tu kufanya.

Ni kweli kwamba watu mbalimbali wana mfanano katika vipaji vyao, au ndoto walizo nazo juu ya maisha yao, LAKINI ukweli ulio wazi ni kwamba, KILA MTU, KILA MMOJA wetu ana uwezo maalum (unique ability) katika kufanya kitu fulani, hata kama watu ELFU MOJA, wanaweza kufanya kitu kama hicho. Ndio maana leo hii tuna mamilioni ya waimbaji lakini, kila mmoja akiimba ni lazima utagundua kuwa fulani ndio kaimba.

Maana yake nini? Ni kwamba katika kile kitu unachoweza kufanya, umebeba package fulani, yenye ladha fulani ya kipekee zaidi inayokutofautisha na watu wengine duniani. Hivyo ukiacha kufanya jambo fulani kwa kuwa watu wengine wanafanya kitu kama hicho, ujue wazi kwamba unaukosesha DUNIA na ULIMWNGU ladha fulani ambayo wanaisubiri kwa hamu Sana.

Tambua ulichokibeba ndani mwako, unachokiweza, kisha anza kufanya na dunia nzima itakushangilia.

Swali ni Je, ni mara ngapi mimi na wewe tumeacha kufanya vitu vya msingi katika maisha yetu, kwa HOFU ya kuwa watu wengine wanafanya vitu kama hivyo?

Tusipofanya Dunia Itakosa Ladha Yetu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment