Unataka Kupandishwa CHEO Na Kuongezwa MSHAHARA Haraka?…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wezi 5 Wanaokuibia Muda Wako Kila Siku Na Namna Ya Kuwakabili

i. Kutoipanga Siku Yako
ii. Kutafuta Vitu Ulivyosahau Ulipoviweka
iii. Maelezo yasiyokamilika
iv. Matumizi Ya Mitandao
v. Mazungumzo / Vikao Visivyopangiliwa

Katika Makala Hii Tutazungumzia Mwizi wa 5

– Mazungumzo / Vikao Visivyopangiliwa

Mwizi wa tano ambaye amewaibia watu wengi sana muda wao ni mazungumzo ambayo hayajapangiliwa.

Mazungumzo haya yanaweza kuwa katika mfumo wa mtu kuja ofisini kwako bila “appointment”.

Mtu kukupigia simu na kutaka muongee hata bila kujua kwa wakati huo uko wapi na unafanya nini…

Vikao vya ghafla kila siku n.k.

Kama nilivyoanza kusisitiza hapo mwanzoni, unatakiwa uwe mtu mwenye uwezo wa kuulinda muda wako.

Ili usitumiwe vibaya aidha na wewe mwenyewe ama na watu wanaokuzunguka.

Kumbuka kuwa watu wengi sana hawaishi kwa ratiba.

Na kwa sababu hiyo huwa hawaheshimu ratiba za watu.

Watu wengi sana hawajali muda na hivyo hawaheshimu muda wa wengine.

Na watu wengi sana hawaishi kwa vipaumbele.

Hivyo hawaheshimu vipaumbele vya wengine.

Moja ya lengo unatakiwa kujiwekea kwenye maisha yako ni kuwa mtu ambaye unaulinda muda wako.

Ili usichukuliwe na watu ambao haukuwapanga kwenye matumizi ya muda wako kwa wakati huo.

Jifunze kuwaambia watu kuwa hautaweza kufanya kitu fulani kwa wakati huo.

Hautaweza kuhudhuria kikao kwa wakati huo.

Au hautaweza kuongea na simu kwa wakati huo.

Kumbuka sio kila simu inayopigwa kila wakati na mtu yoyote ni ya kupokelewa wakati huohuo.

Kuna zingine utawapigia baadae katika muda wako ulioupanga wewe.

Usiruhusu kuwa mtu ambaye muda wako unaingiliwa tu!

Na hakuna unachofanya “Protect Your Time” Linda Muda wako.

Mwanzoni watu watakuchukia na watakusema vibaya.

Ila baadae watajua kuwa ndivyo ulivyo na haitawasumbua tena.

Je, katika wezi hawa watano wewe ni mwizi yupi amekuwa akikuibia muda wako zaidi na unapanga kufanya nini ili kumkabili

Kujifunza zaidi nashauri usome eBook yangu ya “Mbinu Za Kupandishwa CHEO Na Kuongezwa MSHAHARA Haraka”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment