Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mkuu wa NATO anawaleta pamoja Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na viongozi wa mataifa yenye nguvu ya Ulaya mjini Brussels siku ya Jumatano kujadili vita vya Ukraine, wiki chache kabla ya Donald Trump kurejea madarakani.

Mkutano huo wa viongozi unaowajumuisha wale wa Ufaransa, Ujerumani na Poland pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za magharibi, NATO, unafanyika katikati ya miito kutoka Ukraine, ikiwataka washirika wake kuipiga jeki kwenye uwanja wa vita na kidiplomasia kabla ya uwezekano wa kufanyika mazungumzo yoyote na Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atahutubia viongozi wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi , Oktoba 17, akiomba kuwepo kwa “amani ya haki” katika vita na Urusi, huku akihofia kuitwa kuanzisha mazungumzo na Moscow.
Siku ya Jumatatu Oktoba 16, kabla ya kwenda Brussels, Volodymyr Zelensky aliwasilisha mpango wake wa amani uliosubiriwa kwa muda mrefu kwa bunge la Ukraine, ambalo, kulingana na yeye, linaweza kumaliza vita “mwaka ujao”.
Mpango huo una pointi tano, ikiwa ni pamoja na ombi la mwaliko wa kujiunga na NATO na kuongezeka kwa msaada wa kijeshi, pamoja na viambatisho vitatu vya siri vilivyotengenezwa katika wiki zilizopita, baada ya mikutano ya rais wa Ukraine na viongozi wakuu wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Ujerumani.
Kulingana na Volodymyr Zelensky, sehemu ya pendekezo la Kyiv lilikuwa kuanzisha “mfuko wa kuzuia kimkakati usio wa nyuklia” ndani ya Ukraine ili kulinda dhidi ya vitisho kutoka Urusi, lakini hakutoa maelezo yoyote juu ya nini kitahusu.
Badala yake, nchi za Magharibi zitakuwa na jukumu la kuendeleza rasilimali za asili za madini za Ukraine katika siku zijazo, wakati askari wa Ukraine wanaweza kuchukua nafasi ya sehemu za vikosi vya Marekani vilivyoko Ulaya.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.