Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.
Pichani ni Rais wa zambia “Hakainde Hichilema”aliyembwaga Rais wa zamani Edgar Lungu katika uchaguzi uliyofanyika Nchini Zambia
.
Safari yake haikuwa rahisi,Alijaribu zaidi ya Mara 5 bila mafanikio Ila hakukata tamaa
.
Mara ya 1(2006)aligombea na hayati Levy Mwanawasa akashika nafasi ya tatu,alipata asilimia 25 ya kura zote.
.
Mara ya 2(2008) baada ya kifo cha Mwanawasa aligombea tena akashika nafasi ya 3,huku alipata asilimia 19.7
.
Mara ya 3(2011)alishindwa tena kutokana na kuvunjika kwa Muungano wa vyama vya upinzani(UPND na PF) waliouunda ili kupambana na chama tawala.
.
Mara ya 4(2015)aligombea tena na Edgar Lungu Safari hii akapoteza kwa tofauti ya kura asilimia 1 ambazo ni sawa sawa na Kura 27,757,Alishika nafasi ya 2
.
Mara ya 5(August 2016)Alishindwa Tena na Edgar Lungu kwa tofauti ya kura chache sana.
.
April 2017,Alikamatwa na kuwekwa ndani na polisi kwa muda wa miezi 4 na kuachiwa baadaye, kwa amri ya Rais Edgar Lungu.
.
Baada ya kutoka gerezani alipohojiwa katika kipindi cha HARD TALK,alisema”Nilinyimwa chakula na kupigwa bila huruma kwa muda wa siku 8,mke wangu na Rafiki zangu hawakuruhusiwa kuniona”
.
12 August 2021 hii ilikuwa ni Mara ya sita aligombea tena na Edgar Lungu hatimaye mapema tar.16 August alitangazwa kuwa Mshindi wa uchaguzi mkuu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Essau Chulu.
.
Vipi angekata tamaa??leo hii hangekua Rais wa zambia ??
.
Umejifunza Nini kwa “Hakainde Hichilema”?
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.